Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, March 10, 2015

WAFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA WACHANGIA DAMU KWA AJILI YA WATANZANIA WENZAO‏



Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha M-PESA,Gabriel Urasa akiwa amejilaza kwenye kitanda maalum akichangia kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya watanzania wengine. Uchangiaji huo ulifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha Usafirishaji Benworth Komago akitolewa damu na afisa mtoa damu wa mpango wa Taifa damu salama,Peter Chamu wakati wa uchangiaji wa dumu salama iliyochangiwa kwa hiari na wafanyakazi wa kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Afisa mtoa damu wa mpango wa Taifa wa Damu Salama, Daudi Mkawa akimtoa damu mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Lizian Mushi.Wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipojitolea kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya watanzania wengine uchangiaji huo ulifanyika makao makuu ya vodacom Mlimani City jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment