Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, March 3, 2015

CHAMA CHA ALBINO WILAYA YA TEMEKE KULILALAMIKIA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN TANZANIA


Tanzania ni moja ya nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara afrika imekuwa na wimbi la kuongezeka kwa 
watu wenye ulemavu ngozi ,jamii ya kitanzania imekuwa na imani potofu juu ya watu hawa wengine wakiamini
ulemavu wa ngozi ni kama mkosi.
Miaka ya tisini jamii nyingi zilidanganya  ya kwamba albino aishi na iwa wanapotea lakini kweli nikwamba 
jamii hizo zimekuwa zikiwahua pindi pale tu wanapozaliwa na kuwaficha kwa kuwazika katika mashamba na 
hata ndani ya nyumba zao.
Tanzania imeweza kufumbua macho baada ya uhuru wa vyombo vya habari kuanza kuriport habari za mauji
ya watu hawa nakutoa elimu ya kuwatambua albino kama binadamu wengine na wanaweza fanya kila kitu 
kama binadamu wengine.
Lakini miaka ya 2006 yakaanza kutokea mauaji ya watu hawa tena ikishirikishwa na imani za kishirikina 
kwa baadhi ya watu wakiamini wanapotumia viungo vya albino watafanikiwa katika mambo yao ya Biashara
na hata uongozi hasa katika masuala ya siasa.

ndipo harakati za wanahabari kuanza kuliwekea mkazo suala la unyanyasaji wa jamii hiyo ya walemavu wa ngozi
pongezi za dhati ziende kwake Vick mtetema mwanaharakati aliyepigana kufa nakupona kuhakikisha mauaji haya
ya albino yanakwisha nakutokomezwa kabisa ndipo kufanikisha kuanzishwa kwa shirika la "Under the same sun"
ambalo lilikuja kwa nia ya kutetea haki za walemavu hawa na kuwakwamua kiuchumi na hata kielimu.
Lakini licha ya jitiada hizo na walemavu kuwa namategemo juu ya shirika hilo hali imekuwa ndivyo sivyo
baada ya sasa kuonekana shirika hilo likiwa na watu wachache wanaonufaika na misaada hiyo na namba kubwa 
ya watu hao ikibaki ikiwalalamikia viongozi wa shirika hilo Tanzania.



Mwenyekiti wa chama cha Albino(W) ya Temeke Bw; Kassim Kibwe
Akiongea nasi Mwenyekiti wa chama cha albino wilaya ya Temeke Bw.Kassim Kibwe anasema shirika la under
the same sun limekuwa likitenda ndivyo sivyo kwa sasa kama awali lilivyokuja nakutokuwa na imani nalo tena
hasa kwa kitendo cha kusambaza fomu kwa wazazi wasiojiweza ili kuwaandikisha watoto wao waweze someshwa 
lakini ajabu ni kwamba unakuta mzazi hana hata pesa ya kununua kiatu cha mtoto na anaambiwa ampeleke mtoto shule ambazo
ni International na under the same sun wanachangia gharama kiasi na huku gharama zinging zikitakiwa kutoka mzazi tena hugo ambaye 
hana uwezo wa kulimia hata mavazi tu ya mtoto kwa shule za kawaida.

Timu ya Tv51,Fadhagetblogspot wakiwa ofisi za chama cha albino(w)ya Temeke
wa kwanza kushoto Nelson Gama,wa Pili Lonely nzali

Mtoto huyu ni moja ya watoto wanaoitaji kupata Elimu 


mengi utaendelea kuyapata kupitia online Tv51(www.tv51.co.tz)makala na vipindi kama fahamu kuhusu albino
ikiwa pamoja na matatizo yanayowakabili walemavu wa ngozi Tanzania

Na Lonely L.nzali
Dar es salaam

0 comments:

Post a Comment