Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, March 6, 2015

BANZA ALIA KUSHINDWA KUMUAGA KAPT. KOMBA

BAADA ya mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba kuagwa na kusafirishwa kwenda kuzikwa mkoani kwao Ruvuma, msanii wa muziki wa dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amejikuta akilia na kusema ameumia sana kwa kushindwa kwenda kumuaga bosi wake huyo wa zamani kutokana na afya yake kuwa si shwari.


Mwanamuziki Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’.

Akipiga stori na gazeti hili, Banza alisema amehuzunika sana kushindwa kwenda kuuaga mwili wa Kapteni Komba kwani enzi za uhai wake alifanya naye kazi ya muziki kwenye Bendi ya TOT lakini kutokana na afya kuwa mgogoro alishindwa kabisa.

“Imeniuma sana kushindwa kumzika baba yangu Komba maana nilikuwa natamani sana nikamuage mara ya mwisho lakini nikashindwa kutokana na afya yangu kuwa mbaya, Komba nilifanya naye kazi sana na kifo chake kimeniuma mno,” alisema Banza.

0 comments:

Post a Comment