Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, March 18, 2015

MAAMBUKIZI YA FANGASI SEHEMU ZA SIRI -2




WIKI iliyopita tulieleza matatizo ya fangasi sehemu za siri na jinsi wanavyowasumbua waliokumbwa na maradhi haya, tunaeleza ni wanawake gani hupatwa na tatizo hili. Leo tunaendelea kuwaelimisha na tunaanza kufafanua wale wanaopatwa na ugonjwa huu, endelea:

Wengine wanaopatwa na fangasi hawa sehemu za siri ni wale wanaotumia sana dawa za kuua bakteria (antibiotics, steroids) ambazo zina tabia ya kushusha kinga ya mwili.Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini kwa mwanamke husababisha mabadiliko katika sehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa ukuaji wa kasi wa fangasi hawa.

Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili) huweza kusababisha mtu kuwa na fangasi hawa. Hata hivyo, ieleweke hapa kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya.

Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira) au mtu kuwa na upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya Mononucleosis na nk, husababisha mtu kupata maambukizi ya fangasi hawa.

Wengine wanaoweza kuambukizwa fangasi hawa ni wale wenye ugonjwa wa Ukimwi (HIV/AIDS), wanaopata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali au wenye matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi (infertility treatment), wenye utapia mlo (malnutrition), wenye kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kwa muda mrefu kama nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani (chupi) zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nailoni, nguo za ndani zinazobana sana n.k.

Au wale wanaojamiiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi vyenye glycerin wakati wa kujamiana pia yamehusishwa na maambukizi haya.
Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.

0 comments:

Post a Comment