Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, March 17, 2015

MIKE PORCARO AFARIKI DUNIA



Michael Joseph Porcaro enzi za uhai wake.

MWANAMUZIKI Michael Joseph Porcaro amefariki dunia jana kwa Ugonjwa wa ALS akiwa na miaka 59.

Kaka wa Porcaro ambaye walikuwa wote katika bendi ya Toto, Steve aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Mike alifariki dunia kwa amani akiwa amezungukwa na wanafamilia nyumbani kwake Los Angeles, California, Marekani akiwa usingizini.

Mike alijiunga na bendi ya Toto mwaka 1983 akiwa sambamba na kaka zake Steve na Jeff, ila alistaafu mwaka 2007 kutokana na ugonjwa wa ALS.

Mike alipiga gitaa katika nyimbo za bendi hiyo zilizohit kama "Rosanna," "Africa," na "Make Believe."

Ugonjwa wa ALS uliomuua Mike hushambulia seli za mishipa ya fahamu na kupelekea mgonjwa kupata matatizo katika kuongea, kumeza, kupumua na baadaye kupooza.

0 comments:

Post a Comment