Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, March 3, 2015

KABLA HUJAMLAUMU MUNGU KWA MATATIZO YAKO TAZAMA HII

Na Gabriel Ng’osha
WAGOMBANAPO mafahari wawili ziumiazo ni nyasi, haya yametokea kwa Joyce Kauzeni (43) mkazi wa Kibamba, jijini Dar e s Salaam baada ya kupooza sehemu kubwa ya mwili wake, kutokana na mgomo wa madaktari nchi nzima uliotokea Juni, 2012 kwa ajili ya kuishinikiza serikali kutimiza madai yao kumi, likiwemo la masilahi.


Miguu ya Joyce Kauzeni ikiwa imepooza.

Akisimulia mkasa huo mume wa Joyce, Lazaro Mdalamani akiwa nyumbani kwake Kibamba Dar alikuwa na haya ya kusema:

CHANZO CHA TATIZO
“Chanzo cha tatizo la mke wangu kilitokea Juni, 2012 wakati akitokea kanisani. Baada ya kusali alipanda daladala kwenda sokoni maeneo ya Kibamba, akiwa njiani gari kubwa lilifeli breki na kuigonga daladala hiyo likaanguka, mke wangu akapoteza fahamu.“Majeruhi wengine pamoja na mke wangu walikimbizwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha Pwani lakini mke wangu alizidiwa akahamishiwa Hospitali ya Muhimbili.

MGOMO WA MADAKTARI
“Isingekuwa mgomo wa madaktari mke wangu asingekuwa amepooza kwani baada ya kumpeleka Muhimbili, siku chache baadaye ndipo mgomo ukaanza, hakupata huduma stahiki, naamini mgomo umechangia kumfanya apooze.



“Baada ya kupooza alipangiwa awe anakwenda kliniki palepale Muhimbili ili apewe mazoezi lakini sijawahi kumpeleka hata siku moja kutokana na kukosa fedha za usafiri kwani nashindwa kumudu gharama za kukodi usafiri binafsi,” alisema mwanaume huyo.

JANGA LINGINE
Aidha, mume wa mgonjwa huyo aliongeza kuwa, mkewe alilazwa Muhimbili zaidi ya miezi sita na kwa sasa amepata fangasi katika baadhi ya sehemu za mwili wake kwa sababu ya ukosefu wa lishe bora ikiwemo vitamin B.

OMBI MAALUM
Joyce akizungumza kwa shida na gazeti hili alisema: “Ee Mungu, sitembei tena nasubiri kifo changu tu.”
Mama huyo anaomba mtu yeyote aliyeguswa na matatizo yake amsaidie kiasi chochote cha fedha ili aweze kumudu gharama za kwenda kutibiwa Muhimbili.

Kwa kumchangia unaweza kuwasiliana naye kwa simu namba 0765 366824 au 0655207156.


0 comments:

Post a Comment