Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Saturday, February 28, 2015

RECHO APIGA MWEREKA KATIKATI YA SHEREHE

Musa Mateja
MREMBO kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’, amepiga mwereka wa aina yake baada ya kuteleza ukumbini, Risasi Jumamosi limeshuhudia.

Tukio hilo lilijiri juzikati katika Hoteli ya Regence, Mikocheni jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa (bethidei).


Mrembo kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’.

Wakati sherehe ikipamba moto, wageni waalikwa walimmwagia Recho maji na mvinyo kama ishara ya upendo na kusababisha sehemu aliyokuwa amekaa kutapakaa maji.

Wakati zoezi la kummwagia maji na mvinyo likiendelea, katikati ya sherehe, mwanahabari wetu aliyekuwepo ukumbini hapo, alishuhudia mrembo huyo akiteleza na kuanguka chini ambapo wenzake hao hawakujali, wakaendelea kummwagia hali iliyosababisha msanii huyo aangue kilio.




Recho akiwa chini baada ya kupiga mweleka.

“Jamani inatosha, muoneeni huruma kidogo hii sasa si sherehe tena hapa mnamsulubu,” alisikika mmoja wa waalikwa.

Baadaye wageni waalikwa walimfuta Recho maji na zoezi la kukata keki na kulishana kwa ‘staili ya njiwa’ likaendelea huku waalikwa wakiendelea kukata ulabu.


Recho akisadiwa kunyanyuka.

Baada ya shamrashamra kutulia, mwanahabari wetu alimvuta pembeni Recho na kutaka azungumzie sherehe hiyo ambayo katikati ilimfanya aangue kilio: “Nimejikuta tu nikilia na hasa sikutegemea kama wangenimwagia pombe na maji kiasi kile, nywele nilizoweka kichwani zinaniuma sana lakini pia pombe ziliniingia machoni, kimsingi ni jambo la furaha lakini ndiyo hivyo limeniliza,” alisema Recho.
Sherehe hiyo iliwakusanya waalikwa mbalimbali akiwemo shosti yake Recho wa damu, staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linnah’.

KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA


MSIBA MZITO: Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba (pichani), amefariki dunia jioni hii katika hospitali ya TMJ jiijini Dar, mtoto wa marehemu Herman Komba amethibitisha huku akilia. HABARI ZAIDI KUWAJIA HIVI PUNDE.

Friday, February 27, 2015

HOSPITALI YA MUHIMBILI NA CLOUDS MEDIA WAFANYA KAMPENI YA KUCHANGIA DAMU


Sehemu ya damu iliyokusanywa baada ya wananchi kuchangia.




Msanii, Kala Jeremiah akisisitiza watu kujitokeza katika kuchangia damu.…


Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha EFM, Samira Kiango akichangia damu.


Wafanyakazi wa Clouds Media wakiwa kwenye kampeni ya uchangiaji damu.



Baadhi ya wataalamu wakitoa ushauri na huduma kabla ya kuchangia damu.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni.

WAKAZI wa jiji la Dar es Salaam, leo walijitokeza katika zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya waathirika na wahitaji wa huduma hiyo.
Zoezi hilo lilifanyika katika Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Clouds Media, Hospitali ya Muhimbili, Damu Salama na wadau wengine.

Msanii wa Muziki wa Hiphop, Kala Jeremiah amewahimiza wasanii na wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi wanaoaga dunia kwa kutokuwa na damu nyingi katika ajali na kwa kina mama wajawazito.

CHID BENZ: ATOZWA FAINI, AAHIDI KUACHA MADAWA YA KULEVYA



Chid Benz (mwenye shati jeupe) baada ya kuachiwa na mahakama.

…Akiondoka mahakamani.

…Akielekea kwenye gari lililomleta.

MWANAMUZIKI
wa Bongo Fleva, Rashidi Makwilo maarufu kama ‘Chid Benz’, aliyekuwa
anatuhumiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin na bangi, leo
ameachiliwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 900,000.

Katika
maelezo ya awali yaliyosomwa na mwendesha mashtaki wa Jamhuri Diana
Lukendo, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, msanii huyo alimwambia
hakimu kuwa mshtakiwa alikamatwa na dawa hizo za kulevya akiwa Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, akitaka kusafiri
kuelekea mkoani Mbeya.

Hata hivyo mshtakiwa huyo ambaye alikiri
kosa mnano tarehe 18 Aprili mwaka huu, leo aliiomba mahakama
kumpunguzia adhabu na kwamba asingetumia tena ulevi huo na
atawaelimisha vijana wenzake juu ya madhara yake.

WATATU WANUSURIKA KUFA KWA AJALI MWANZA





Mwonekano wa gari hilo baada ya kupata ajali.




Wasamaria wema wakitoa msaada.


Mashuhuda wakiwa katika eneo la tukio.

GARI dogo aina ya Toyota RAV4 limepinduka leo katika kijiji cha Mbela wilayani Misungwi, mkoani Mwanza na kujeruhi watu kadhaa waliokuwa ndani yake baada ya kumshinda dereva wake wakati lilikata kona na hivyo kuanguka katika bonde la daraja.

Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo lenye usajili wa T 358 CBA mali ya Machalo Joseph, lilikuwa likiendeshwa na Festo Kakula wa Misungwi, na baada ya ajali majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Mitindo wilayani Misungwi.

Thursday, February 26, 2015

DADA WA AFANDE SELE AFIA GESTI


Dustan Shekidele, Morogoro
DADA wa msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ Zaria Kambi (30) ambaye alikuwa ni mhudumu wa baa, amekutwa ameuawa kikatili katika Gesti ya Stavi (Gesti ya Marafiki) iliyopo Kichangani, mjini Morogoro.


Dada wa msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ Zaria Kambi.

Tukio hilo la kinyama lilitokea usiku wa Jumapili iliyopita baada ya marehemu kuwa amekubaliana kulala pamoja na mteja aliyekuwa akimhudumia kinywaji, ambaye pia alikuwa amechukua chumba katika nyumba hiyo hiyo iliyokuwa na baa.

Kwa mujibu wa rafiki wa marehemu, ambaye pia alikuwa ni mhudumu wa gesti hiyo, Rehema Saleh, alisema mtu mmoja asiyefahamika, alifika kazini kwao na kupanga chumba namba 8A na baadaye alienda upande wa baa kunywa pombe akihudumiwa na Zaria.

“Mimi na Zaria (pichani) tunaishi jirani, sasa baada ya kumhudumia na yeye kununuliwa pombe, wakakubaliana walale pamoja, tunaishi jirani hivyo kila siku baa ikifungwa tunaongozana na jana tuliongozana njiani aliniambia amepata kichwa hivyo anakwenda nyumbani kuaga na baadaye arejee kwa bwa’nake huyo ambaye ni mara ya kwanza anaonana naye,” alisema Rehema na kuongeza.

“Cha ajabu saa 8 usiku napigiwa simu na mlinzi akidai Zaria amenyongwa na mteja wake, sikuwa na jinsi, kulipokucha nilifika hapa gesti na kukuta mwili wa marehemu ukiwa akitandani,” alisema na kuangua kilio.


Chumba cha Gest alichokutwa amekufa Zaria Kambi.

Mlinzi wa gesti hiyo, John Emmanuel akizungumzia tukio hilo, alisema majira ya saa 6 usiku Zaria aliingia katika chumba namba 8A na saa moja baadaye, akasikia kelele zikitoka chumbani humo, ambazo alihisi ni za kimapenzi.

“Sijakaa vizuri saa 8 usiku jamaa alitoka na begi lake akitaka nimfungulie aondoke huku mkononi akiwa na tiketi ya basi kuelekea Mbeya, nikamwambia kwanza twende chumbani kwake nikachunguze ndipo nimruhusu atoke, awali aligoma na mimi nikagoma kumfungulia geti, tukaganda kama dakika mbili akakubali kwenda chumbani tulipofika tukamkuta Zaria amekufa huku akiwa mtupu, nikamjulisha bosi Pascal Mafikiri ambaye aliita polisi wakamchukua mtuhumiwa na mwili wa Zaria,” alisema.

Mama mzazi wa marehemu, Mwajuma Hassani Kambi ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mwande Kata ya Kichangani kwa tiketi ya Chadema alipokea taarifa za kifo cha mwanaye Jumapili usiku.

Alisema mwanaye ameacha mtoto anayeitwa Rashid lsmail Kaliembe ambaye anasumbuliwa na uvimbe tumboni na kwamba kila mwezi alikuwa akipelekwa Muhimbili kwa matibabu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa, Erick Bruno, ambaye ni mkazi wa Manzese Tip Top Dar es Salaam, anashikiliwa. Marehemu huyo alizikwa Jumanne iliyopita mjini Morogoro.

DR. FADHIL EMILY: MAGONJWA SUGU HAYANA NAFASI KWET



Designer: Rumafrica

MWANDISHI ALBINO ANUSURIKA KIFO MARA MBILI

OJUKU ABRAHAM/Amani

MWANDISHI wa habari mwandamizi, Henry Mdimu ambaye ni Albino, aliyejiteua kuwa Balozi wa kuwatetea walemavu wa ngozi kwa kuanzisha kampeni aliyoiita Imetosha, kutokana na kukithiri kwa mauaji dhidi yao, amesema alinusurika kuuawa mara mbili na watu alioamini walihitaji viungo vyake, Amani lina data kamili.

Mwandishi wa habari mwandamizi, Henry Mdimu.

Akizungumza na gazeti hili juu ya nia yake hiyo ya kujitolea kupinga mauaji hayo anayotegemea kuwatumia zaidi wasanii wa muziki wa kizazi kipya ili wapaze sauti zao, alisema siku zote hakuwahi kudhani kama tishio hilo ni kubwa na hata aliponusurika mara ya kwanza akiwa mkoani Dodoma, bado hakuamini.

“Nilikuwa Dodoma natoka muziki usiku, nikachukua teksi ili inirudishe hotelini nilikofikia, mara ndani ya teksi wakapanda watu wengine wawili, sikujali nikajua ni mashanta, sasa nikashangaa mwelekeo wa gari ni tofauti na nilivyowaelekeza, nikaanza kubishana nao. Nilivyoona hivyo, nikampigia simu rafiki yangu niliyemuacha disco, nikaiacha simu wazi ili asikie kinachoendelea ndani ya gari, baadaye nikamwambia nipo maeneo ya stendi, akaniambia anakuja.

“Sasa tukawa tumesimama tunabishana, mara rafiki yangu akatokea akiwa na mtu mwingine, wakasaidiana kunishusha nikaendelea na safari zangu,” alisema Mdimu, baba wa mtoto mmoja, ambaye pia ni blogger.

Tukio la pili lililohatarisha maisha ya mwandishi huyo, ambaye pia amewahi kufanya kazi Global Publishers, ambalo analielezea kuwa ndilo lilikuwa hatari zaidi, lilimtokea mkoani Mbeya, alikokuwa amekwenda kwa shughuli zake za kikazi na kufikia katika hoteli moja ambayo ameisahau jina.

“Nilikuwa chumbani kwangu nikapigiwa simu na mapokezi wakaniambia kuna wageni wako. Nikatoka na kuwakuta watu ambao siwajui, waliojitambulisha kama mashabiki wangu wanataka tuongee.

Basi tukakaa sehemu ya kinywaji tukaanza kupata, sasa kumbe ikawa kila nikienda chooni kujisaidia, wao wanajifanya kuzungumza ili kuwazuga watu eti kwamba mimi ni mtu wa Mbeya lakini nakataa kwenda kwetu na hawajui watanishawishi vipi ili siku hiyo niondoke nao,” alisema.

Mdimu alisema mara ya mwisho alipokwenda chooni, mmoja wa wahudumu alimfuata na kumwambia akirudi mezani asinywe kinywaji chake kwa sababu wale watu waliweka kitu kibaya, jambo lililomtisha na kuwaomba wawaite polisi ambao walikuja na kuwakamata watu hao ambao walishindwa kujieleza. “Waliwachukua na kuondoka nao, sikuwahi kufuatilia kilichoendelea,” alisema Mdimu na kuongeza kuwa mauaji ya hivi karibuni ya mtoto huko Geita, yamemfanya sasa kutambua hatari kubwa iliyo mbele yao na kuomba jamii kuungana ili kuwaangamiza wahalifu hao.

MISS UNIVERSE NALE BONIFACE ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) CHA SALVATION ARMY JIJINI DAR ES SALAAM



Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akikata keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvation Army jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.
Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akiwalisha Keki na wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvation Army jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.

Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvation Army jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.

Sehemu ya wanafunzi wenye matatizo ya Ngozi (ALBINO) katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvation Army jijini Dar es Salaam.

Miss Universe Tanzania 2014-2015 Nale Boniface akigawa madaftari kwa wanafunzi wenye mahitaji wakati alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Salvation Army jijini Dar es Salaam ikiwa ni madhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliamua kuwapelekea zawadi watoto hao.

Wednesday, February 25, 2015

MSHITUKO WA MOYO (MYOCARDIAL INFARCTION)




Mshituko wa moyo unatokea wakati mtiririko wa damu yenye oksijeni unapozuiwa kwa ghafla katika misuli ya moyo. Iwapo mzunguko huo wa damu hautaendelea haraka, kitendo hicho huifanya misuli ya moyo kuharibika kwa kukosa oksijeni na hivyo kuhatarisha maisha ya muathirika.

Mshituko wa moyo kwa lugha ya tiba unajulikana kama ‘Myocardial Infarction’ inayomaanisha “Myo” muscles au msuli, ‘cardio’.... Heart au moyo na “infarct”....kufa kwa tishu kutokana na kukosa oksijeni.
Kama vilivyo viungo vingine mwilini hasa misuli, moyo nao huhitajia damu.

Bila damu seli za moyo hudhoofika suala linalosababisha mtu kuhisi maumivu. Mshituko wa moyo au Heart Attack kama hutaki kutumia myocardial onfarction, hutokea pale mshipa mmoja wa damu au zaidi inaposhindwa kusafirisha damu yenye oksijeni katika moyo, kutokana na kuziba mishipa hiyo.

Mishipa ya damu inaweza kuziba kwa sababu tofauti kama vile, kuta za mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo (coronary arteries) kuwa nene, chembechembe za mafuta kujikusanya katika mishipa ya damu, kudhoofika na kukonda mishipa ya damu, mishipa ya damu inaposinyaa na kushikana au spasm na kujitokeza donge la damu katika mishipa ya damu.

Mshituko wa moyo mara nyingi husababishwa na ugonjwa wa moyo wa mishipa ya damu au Coronary Heart Disease (CHD). Hii ni hali ambayo ndani ya mishipa ya damu hutokea kitu kiitwacho ‘plaque’ na kuzuia damu isiweze kupita katika mishipa ya damu, ambayo ni matokeo ya muda mrefu. Lakini ni wakati gani mtu hukabiliwa na hatari ya kupata mshituko wa moyo?

Ni pale umri wa mtu unapoongezeka na kuwa mzee, mtu anapokuwa na unene wa kupindukia, kuvuta sigara, kuwa na shinikizo la damu au High Blood Pressure. Kuishi bila kuwa na harakati na kutoushughulisha mwili.

Mtu kuwa na kiwango cha juu cha mafuta katika damu au High Blood Cholesterol. Kuwa na ugonjwa wa kisukari na kuwa na msongo wa mawazo, wasiwasi na fikra nyingi. Mambo mengine yanayochangia kupata mshituko wa moyo ni baadhi ya magonjwa ya moyo, kufanyiwa upasuaji wa moyo, kuwa na ndugu katika familia ambao wana matatizo ya moyo na jinsia ya kiume.

Uvutaji sigara husababisha mshituko wa moyo unaotokana na kuziba mishipa ya damu kwa asilimia 36, ambapo unene husababisha ugonjwa huo kwa asilimia 20. Kukaa bila kujishughulisha au kufanya mazoezi husababisha mshituko wa moyo kwa asilimia 7-12. Pia wanaume wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo zaidi kuliko wanawake katika kipindi chote cha maisha hasa kabla ya wanawake hawajafikia wakati wa kukatika hedhi. Lakini kwa ujumla kwa kuwa wanawake huishi miaka mingi kuliko wanaume, magonjwa mengine ya moyo husababisha vifo vya wanawake uzeeni zaidi kuliko wanaume.

WASTARA AZIMIA KISA MAPENZI

Waandishi wetu/Mchanganyiko
DIVA wa filamu nchini, Wastara Juma ambaye kwa sasa anaripotiwa kuwa katika mapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Bin Suleiman anadaiwa kupoteza fahamu mara tu baada ya kupewa taarifa kuwa mpenziwe huyo amepata mtoto wa nne kwa mwanamke mwingine, Risasi Mchanganyiko linakupa stori kamili.

DIVA wa filamu nchini, Wastara Juma akiwa hospitali baada ya kuzimia.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara alipenyezewa ubuyu na mpenzi wa zamani wa Bond, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na kuambiwa kwamba asijishebedue kwani Bond ana mwanamke mwingine ambaye amejifungua mtoto wa nne hivi karibuni.

“Tunakushangaa unavyojinadi kuwa Bond ni wako na kumpa zawadi ya keki ya bethidei wakati mwenzako amezaa na mwanamke mmoja baamedi hivi karibuni. Tena si kwamba mtoto huyo ni wa kwanza, ni wa nne,” kilisema chanzo hicho kikimnukuu Aunty.

ALIVYOZIMIA
Chanzo hicho kifunguka kuwa, baada ya kupewa taarifa hizo na Aunty Lulu, alizimia ghafla na kulazwa hospitali.“Wastara alizimia punde tu baada ya kupewa taarifa hizo, nasikia walimkimbiza hospitali, akapewa huduma nasikia kidogo sasa hajambo. Ishu ilikuwa mbaya, Aunty Lulu alimmchana laivu.”

Wastara Juma akiwa na Bond Bin Suleiman.

AUNTY LULU ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Aunty Lulu ambaye hapo awali alikuwa akilalamikia penzi la kitumwa la kupigwa mara kwa mara na Bond na hata kufikia mahali na kushukuru Mungu kwa kutengana kwao na kumuuliza kama habari hizo zilikuwa na ukweli wowote.

“Ni kweli nilimwambia kila kitu Wastara na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa ili kujua kama kweli ni wa Bond.“Mimi niliamua kufunguka baada ya Bond kunitukana na kunitolea maneno mazito, kwani nilichoka, kama amepata presha na kulazwa hilo mimi silijui,” alisema Aunty Lulu.

TUJIUNGE NA WASTARA
Kwa upande wake, Wastara naye alikiri kupoteza fahamu na kulazwa hospitalini, lakini akakataa mambo hayo kumtokea kwa sababu ya kusikia taarifa hizo, bali kutokana na kuzidiwa na malaria.


“Nimepata nafuu na nimeshatoka hospitali, nilikuwa nimepatwa na homa kali ya malaria, madaktari waliniambia nilikuwa na malaria 10, kwa muda wa wiki mbili nilikuwa naumwa, lakini nikazidiwa kidogo, hivi sasa niko sawa na hapa ndiyo nashuka uwanja wa ndege natokea Mwanza,” alisema.

AMEKWEPA VIUNZI?
Mwanahabari wetu alipombana zaidi Wastara kutaka kujua kuzimia kwake kama kulitokana na kupata habari za Bond kuwa na watoto wanne, alisema siyo kweli kwani asingeweza kushangazwa na jambo hilo hasa kwa vile Bond ni mwanaume lijali na pia ana maisha yake ambayo hayamhusu. “Mimi nina maisha yangu, yeye ana maisha yake, sasa jamani mimi nitapatwaje na presha kwa mambo hayo? Labda nikuambie tu kuwa hakuna lolote linaloendelea kati yangu na yeye zaidi ya masuala ya kikazi tu. Ninaomba uelewe hivyo kwa sababu huo ndiyo ukweli,” alisema.

WATU WATANO WANUSURIKA KIFO AJALINI MWANZA



Muonekano wa mbele wa gari hilo lililopata ajali.

Muonekano wa chini ya gari baada ya kupinduka.




Matofali yaliyokuwa kwenye gari hilo yakiwa yamemwagika chini.

WATU watano (5) wamenusurika kifo ajalini baada ya gari walilokuwa wakisafirishia matofali kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara kisha kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni katika Kijiji cha Ng’ombe wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza ambapo gari hilo aina ya Fuso lenye namba za usajili T726BMY mali ya Sanne Shimbe, lilikuwa likiendeshwa na tajiri huyo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari hilo lilikuwa kasi, tairi ikapasuka hivyo gari likapoteza uelekeo na kuacha barabara kisha kupinduka.

“Gari lilikuwa kasi hivyo baada ya tairi kupasuka lilitoka barabarani na kuingia kwenye matuta ya viazi vitamu likakwama ndipo likapinduka,” alisema shuhuda.
Kwa upande wake dereva Shimbe, alisema baada ya tairi kupasuka alijitahidi kulizuia gari hilo lisianguke lakini ilishindikana. “Nilijitahidi kuliweka sawa gari barabarani baada ya tairi kupasuka lakini ilishindikana kabisa ndio likatoka barabarani na kupinduka lakini nashukuru Mungu tumetoka wazima.
“Tulikuwa watano, mmoja wetu ndiyo ameumia mguu na ameshapelekwa hospitali, anaendelea vizuri, sisi wengine hatukupata majeraha,” alisema Shimbe.

Tuesday, February 24, 2015

MAITI YA MCHUNGAJI REGINALD MHANDO YAZUA TAFRANI

Na Haruni Sanchawa/Uwazi
MAITI ya Mchungaji James Regnald Mhando aliyefariki Februari 18, mwaka huu imezua tafrani nzito kwa ndugu na jamaa baada ya kujulikana kuwa alikuwa na wake wawili ambapo mke mmoja alitaka mwili uagwe hospitali na upande wa pili ukitaka ukaagwe kwa mama yake marehemu.


Mchungaji James Regnald Mhando enzi za uhai wake.

Katika msiba huo ilibainika kuwa, mchungaji huyo (kanisa lake tunalihifadhi kwa sababu maalum), alikuwa na watoto sita kwa mama tofauti na wote walijitokeza katika mazishi ya baba yao.

Inadaiwa kuwa Mchungaji Mhando alianza kuumwa Jumamosi ya Februari 14, mwaka huu lakini inadaiwa baadhi ya watoto na ndugu wengine hawakujulishwa hadi Jumanne ambapo inadaiwa alibebwa na gari la wagonjwa kutokea Morogoro hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Jeneza la mchungaji James Regnald Mhando.

Habari zinasema ilipofika Jumatano saa tano usiku, mchungaji huyo aliaga dunia na mbali ya kuaga dunia, bado tukio hilo lilikuwa ni siri na ilidaiwa ilikuwa afanyiwe shughuli za mazishi kwa siri bila ya baadhi ya watoto wake wakubwa kujua.

Hata hivyo, habari za msiba huo zilizagaa haraka na kumfikia mke wa kwanza wa ndoa ambaye alikuwa nchini kwa ajili ya mapumziko kwani anafanya kazi nje ya nchi, hivyo ukoo ukaanza kutaarifiana.

Mchungaji Mhando alioa na kufunga ndoa Novemba 17, 1979 katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, jijini Dar es Salaam, hata hivyo, ilidaiwa kuwa mwaka 1985 mtumishi huyo wa Mungu aliamua kuondoka nyumbani alikokuwa akiishi na mkewe na kwenda kuishi na mwanamke mwingine ambaye inadaiwa kuwa alikuwa ni wa dhehebu lingine na wakafunga ndoa serikalini.

Habari zinadai kwamba mwanamke huyo alikuwa anaitwa Mwanaheri kabla ya kubadili dini na kuitwa Glory na wakafanikiwa kuzaa watoto wawili, mmoja akapewa jina la Reginald Junior na mtoto mwingine anaitwa Sada au Doreen Mhando. Habari zinasema kabla ya kuondoka kwa mke wa kwanza, mchungaji huyo alizaa naye watoto wawili, wa kiume na wa kike.
...Askari akiwa eneo la tukio.

Hata hivyo, wakati wa msiba huo watoto wengine wawili walijitokeza nao wakidai kuwa ni baba yao, hali iliyozusha minong’ono kwa watu walioshangazwa na mwenendo wa marehemu.Akizungumza na Uwazi, mama mzazi wa mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Dorofea Mhando (82) alisema kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo ni kibaya kwani alimshawishi mwanaye kuisaliti familia yake.

“Mwanamke huyo mwingine alikuwa akiishi na mwanangu kwa siri kubwa sana, kama vile marehemu hakuwa na familia na akawa anajifanya kuwa yeye ndiye mke wa kwanza, kitu ambacho ni cha uongo kwani marehemu alishaoa kanisani mwaka 1979.

“Marehemu baada ya kumpata mwanamke huyo alikuwa hashiriki shughuli nyingi za hapa nyumbani kwa kuhofia watu watajua kuwa alikuwa na familia nyingine, kitu ambacho kilinisikitisha,” alidai mama huyo.


Mwili wa marehemu ukiagwa.

Mama huyo aliongeza kuwa maisha ya mchungaji huyo yalikuwa sehemu mbili, Morogoro na jijini Dar es Salaam, alikuwa akifikia Mivinjeni kwenye ofisi ya shughuli zake.“Baada ya kupata taarifa ya msiba niliagiza mwili uletwe hapa Ukonga Majumba Sita ukitokea Muhimbili kwa ajili ya shughuli za kuagwa lakini mke mdogo akawa anapinga,” alidai mama huyo.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa mke mdogo alisisitiza kuwa baada ya kuandaa mwili wa marehemu uagwe Muhimbili, kisha upelekwe katika Makabauri ya Kinondoni kwa mazishi. Kulitokea mabishano ambapo mtoto mkubwa wa marehemu aliyefahamika kwa jina Feda, alisema baba yao hawezi kuagwa kama mkimbizi kwani ana watoto, mke na mama yake mzazi, hivyo akaamuru mwili ukaagwe kwa bibi yake Ukonga Majumba Sita.

Habari zinadai kuwa mvutano huo ulifikishwa Polisi Kituo Kikuu ambapo lilifunguliwa jalada namba CD/ RB/ 2627/ 2015 ambao waliamuru shughuli za mazishi zisifanyike hadi muafaka upatikane.
Habari zinadai kikao kilifanyika polisi na muafaka ukapatikana kwamba mwili ukaagwe kwa mama yake mzazi Ukonga Majumba Sita.
Maofisa wa polisi walitoa askari wenye silaha chini ya kamanda wao aliyefahamika kwa jina moja la Manyama aliyeongozana na wana familia hao hadi Muhimbili kisha Ukonga, baadaye kwenye Makaburi ya Kinondoni ambapo mchungaji huyo alizikwa chini ya ulinzi.

Monday, February 23, 2015

MAZISHI YA FAITH CATHERINE GONDWE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM


Umati mkubwa wa waombolezaji wamejumuika na familia ya Mzee Geofrey Gondwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele Marehemu Faith Catherine Gondwe, dada yetu aliyeaga dunia ghafla Jumanne iliyopita nyumbani kwao Baahari Beach jijini Dar es salaam. Ujumbe wa sauti wa kurekodiwa kutoka kwa Mzee Gondwe ambaye yuko India kwa matibabu kuliwaliza wengi na wakati huo huo uliwafariji pale aliposema "Kufariki dunia kwa Faith ni mapenzi yake Mungu"
Ibada ya mazishi ikiendelea.

Shada maalumu kwa Faith.

Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathia Chikawe, Profesa Amandina Lihamba akiweka shada la maua kwa niaba ya familia yao ambao ni ndugu wa karibu na familia ya Gondwe.

Wanachama wa Jambo Group ambao ni marafiki wa karibu wa baba wa marehemu wakiweka maua kaburini.

Marafiki waliosoma na Marehemu Faith nchini India wakiweka maua kaburini.