Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, February 16, 2015

AINGIZWA MOCHWARI AKIDHANIWA AMEKUFA

Na Imelda Mtema
Kijana mmoja, Omary Ramadhani, 28, (pichani) mkazi wa Sinza Madukani, Dar amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya kugongwa na ‘Break Down’ alipokuwa akiendesha Bajaj katika makutano ya Barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi, Mwenge, jijini Dar es Salaam.


Kijana Omary Ramadhani anayedaiwa kuingizwa mochwari akidhaniwa amekufa.

Akizungumza kwa masikitiko, Omary alisema kuwa alipogongwa na gari hilo hakuweza kujitambua kwani hata wasamaria wema walivyomchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walijua alifariki dunia hivyo wakamuingiza moja kwa moja mochwari, lakini kwa bahati nzuri alitokea nesi mmoja aliyeshauri asiwekwe kwanza kwenye friji mpaka apimwe.

Akiendelea kuzungumza kwa tabu kutokana na maumivu ambayo anayo, Omary alisema baada ya nesi huyo kumpima aligundua alikuwa akipumua kwa shida.

Alisema hata ndugu zake walijua ameshafariki dunia kutokana na alivyokuwa, kwani alivunjika mgongo mara sita na mfupa wa mkono ulitoka nje na kupasuka kichwani jambo lililosababisha kuvuja damu nyingi.

Alifafanua kuwa kutokana na hali yake, alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo baada ya siku tatu alizinduka na walipokuja ndugu zake aliwauliza alikuwa wapi, walipomuambia Muhimbili alizimia tena.

0 comments:

Post a Comment