Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, February 8, 2015

PIKIPIKI YATEKETEA KWA MOTO UBUNGO JIJINI DAR

PIKIPIKI iliyokuwa ikitokea Kimara imegongana na daladala aina ya DCM inayofanya safari zake kati ya Mbagala - Ubungo mchana huu eneo la Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea wakati pikipiki na DCM vikivuka mataa hayo ambapo pikipiki imeingia uvunguni mwa DCM na kukokotwa huku ikitoa cheche zilizopelekea moto kuwaka na pikipiki hiyo kuteketea kwa moto. Aidha sehemu ndogo ya daladala hilo nayo ilishika moto wakati pikipiki ikiteketea.

Imeelezwa kuwa dereva wa pikipiki hiyo ameumia sana na hali yake ni mbaya kutokana na majeraha aliyoyapata.



Wananchi wakishuhudia pikipiki iliyoteketea kwa moto baada ya kugongana na daladala eneo la Ubungo Mataa mchana huu.


Dalaldala aina ya DCM linalofanya safari zake kati ya Mbagala - Ubungo baada ya kugongana na pikipiki iliyoteketea.




Pikipiki ikiwa imeteketea baada ya kugongana na DCM kisha kuingia uvunguni mwake na baadaye kuteketea kwa moto mchana huu.

0 comments:

Post a Comment