Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, February 20, 2015

ESAMI YATIA SAINI MKTABA WA MRADI WA ZAIDI YA DOLLA MIL.500 KUSAIDIA VIJANA TANZANIA

Wizara ya Habari,vijana utamaduni na michezo kupitia wizara ya michezo leo imetia saini na shirika la ESAMI ya makubaliano yenye lengo la kuwakwamua vijana kiajira kupitia sekta ya ujasirimali.

Akitia saini mkataba huo Katibu mkuu wizara ya vijana leo hii katika jengo la Golden tower ukumbi wa JB Belmonte Jijini Dar es salaam.

Bi Siana Singa na Kurugenzi wa ESAMI Prof;Mwape amesema mradi huo wa Takriba dola za kimarekani zaidi ya milioni 500 zitatia chachu kwa vijana kupata mafunzo ya ujasiriamali hapa nchini na baadae waweze kujiajiri na hata kuwapatia ajira wenzao.


Katibu wizara ya vijana Bi Singa(kushoto) na Mkurugenzi wa ESAMI Prof;Mwape wakitia saini makubaliano katika hotel Ya JB Belmonte (Dar es Salaam.

Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ni moja ya nchi zilizo na uhaba wa ajira kwa takribani asilimia 75% kwa nchi zilizokusini mwa jangwa la sahara,hivyo kupitia mradi huu vijana wataweza kujikwamua na ujasilimali hapa nchi.

akiongeza katika hotuba yake waziri wa Habari,vijana utamaduni na michezo MH;Dk Fenella Mukangara amesema mpaka sasa wajasiliamli hapa nchi hawajaweza kuvuka mipaka ya kmataifa ya bidhaa zao kuweza kuuzwa kimataifa.

Hivyo kupitia mpango huu vijana watawakilisha mawazo yao na kisha watapewa mafunzo yakuboresha biashara zao ziweze kuuzwa nje ya nchi zao na hata kimataifa.

Waziri wa Habari, vijana utamaduni na michezo Mh:Dk Fenelle Mukangara akifungua mradi wa ESAMI

Shirika la Esam limekuwa likifanya mradi huu wa kuwawezesha vijana kwa Takribani nchi 26 barani afrika lengo likiwa ni kuwakwamua vijana na janga la ajira barani Afrika.

Mh:Dr Fenella Mukangara akisalimiana na Dr.Fadhil Emily wa The Fadhaget Sanitarium clinic na Mkurugenzi wa Fadhaget Media katika makubaliano hayo ambaye ni mmoja wa wadau wa maendeleo ya vijana nchini.

Mkurungezi wa Shirika la ESAMI Prof ;Mwape akitoa muongozo na Malengo ya shirika hilo hapa nchini

vijana si taifa la kesho kama waenga walivyosema bali nitaifa la leo ,hivyo ni jukumu la kila mtanzania kuwapa nafasi vijana ilikuweza kuitengeza kesho .

Na:Lonely Nzali(Television 51)

0 comments:

Post a Comment