Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, April 18, 2014

JE UNAFAHAMU DALILI NA ISHARA ZA UJAUZITO? THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUPA JIBU

Doctor Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic ninependa kukusalimu kwanza na pole kwa majukumu yanayokusibu. Leo hii nilitaka ujue ya kwamba dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana

Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kuelezea au kutofautisha matatizo mengine mbali ya ujauzito.

Dr. Fadhili Emily

Dalili na ishara za Ujauzito:


1. Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii

2. Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa za ujauzito
3. Maumivu ya matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
4. Uchovu, wanawake wengi hujihisi uchovu na hali ya kutopenda kufanya lolote.
5. Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
6. Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
7. Kichefuchefu na kutapika
8. Maumivu ya kichwa
9. Kizunguzungu
10. Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
11. Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
12. Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
13. Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
14. Tumbo kujaa au kuvimbiwa
15. Kununa na kukasirika haraka
16. Kiungulila au kupata choo kigumu
17. Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
18. Kuongezeka uzito
19. Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)
20. Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
21. Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii huitwa pia Chadwick's sign

Dalili nyingine ni pamoja na


1. Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)
2. Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
3. Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
4. Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
5. Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto
6. Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound

2 comments: