Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, April 14, 2014

THE FADHAGATE SANIATARIUM CLINIC INAKUPA SOMO LA SHINIKIZO LA DAMU/HIGH BLOOD PRESSURE/HYPERTENSION

Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic ningependa nikusalimu na kama ni mgonjwa nikupe pole na mateso unapata

Kabla ya yote ningependa kutoa utangulizi wa Shinikizo la damu kwa kawaida husababishwa na kuongezeka msukumo wa damu katika kuta za mishipa ya damu, hali ambayo huufanya moyo ufanye kazi zaidi kuliko kawaida ili kuzungusha damu mwilini. Shinikizo la damu huanishwa na namna damu inavyopiga kwenye kuta za mishipa ya damu. Kwa kawaida shinikizo la damu la mtu hupanda na kushuka kila siku, kwa baadhi ya watu hubakia juu na hapo ndipo huambiwa kuwa wana shinikizo la juu la damu. Ugonjwa huu kwa kawaida huitwa muuaji wa kimya kimya kwa maana kuwa, mtu anaweza akawa na ugonjwa huo kwa miaka kadhaa lakini bila kujua, huku ugonjwa huo ukimletea madhara makubwa. Njia ya pekee ya kujua iwapo una ugonjwa huu, ni kwenda kupimwa shinikizo lako la damu. Hii ni kwa sababu shinikizo la damu lisilodhibitiwa huathiri na kuharibu moyo, macho na figo na huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kiharusi.

Shinikizo la damu au presha huonyeshwa kwa muhtasari wa vipimo viwili vya sistoli na dayastoli, ambapo sistoli ni kipimo cha damu kinachopima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo ukidunda, na diyastoli ni kipimo cha damu kinachopima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo umepumzika au kati ya mapigo ya moyo. Shinikizo la damu hupimwa katika milimeta mercury. Kiwango cha kawaida cha msukumo wa damu pale mwili unapokuwa haupo katika harakati huanzia sistoli 100 hadi 140 mmHg na diyastoli 60 hadi 90 mmHg. Shinikizo la juu la damu ni pale vipimo hivyo vinapozidi mmHG 140/90.

AINA ZA SHINIKIZO LA DAMU

Shinikizo la damu limegawanyika katika makundi mawili, ambayo ni
  • shinikizo la damu aina ya kwanza ambalo kitaalamu huitwa primary au essential hypertension. Aina hii ya shinikizo la damu huwapata asilimia 90 hadi 95 ya wagonjwa, huku sababu zikiwa hazijulikani suala linalomaanisha kuwa wagonjwa huwa hawana sababu za wazi zinazosababisha tatizo hilo.
  • Kesi zinazobakia za shinikizo la damu ambazo ni asilimia 5-10 za wagonjwa husababishwa na shinikizo la damu aina ya pili, na kitaalamu huitwa secondary hypertension. Aina hii husababishwa na sababu mbalimbali zinazotokana na matatizo ya figo, mishipa ya damu, moyo na mfumo wa endocrine. Shinikizo la damu kwa kawaida huongezeka katika kipindi cha miaka kadhaa na huweza kumpata karibu kila mtu, lakini huwapata zaidi watu wazima wenye umri wa zaidi ya miaka 35. . Sababu nyingi huathiri ugonjwa wa shinikizo la damu kama vile kiwango cha maji mwilini, kiwango cha chumvi mwilini, homoni, mishughuliko ya mtu, hali ya joto au hali ya baridi, hisia, hali ya figo, mfumo wa neva na mishipa ya damu. Iwapo shinikizo la damu litakuwa juu na kuachwa bila kudhibitiwa, moyo na mishipa ya damu kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Kwa bahati nzuri, shinikizo la juu la damu ni rahisi sana kugunduliwa, kutibiwa na kudhibitiwa.
SABABU ZA TATIZO LA SHINIKIZO LA DAMU

Kuna sababu nyingi na zinazotofautiana kulinga na aina ya ugonjwa huo. Katika aina ya kwanza ya shinikizo la damu ingawa chanzo huwa hakijulikani, lakini sababu za kijenetiki na za kimazingira kama chakula na mazoeni zina nafasi muhimu katika usababishaji wa ugonjwa huo. Hivyo masuala yafuatavyo yamehusishwa katika kusababisha aina hii ya shinikizo la damu. Masuala hayo ni uvutaji sigara, unene (visceral obesity) yaani unene wa sehemu za tumbo, unywaji pombe, upungufu wa madini ya potassium, upungufu wa vitamin D, kurithi, umri mkubwa, chumvi na madini ya sodium kwa ujumla, ongezeko la kemikali kwenye figo (renin) na kushindwa kufanya kazi kichocheo cha insulin. Aina ya Pili ya shinikizo la damu husababishwa na tatizo lililopo mwilini. Matatizo hayo ni pamoja na kasoro ya kuzaliwa nayo katika mshipa mkubwa wa damu, saratani ya figo, saratani ya tezi iliyo juu ya figo, hali ya kushindwa kupumua vyema usingizini (sleep Apnea), ujauzito ambapo baadhi ya akina mama wajawazito hupata shinikizo la damu suala linalosababisha hatari ya kupata kifafa cha mimba (eclampsia), na pia magonjwa ya figo kama vile mshipa wa damu wa figo kuwa mwembamba yaani renal artery stenosis, matumizi ya baadhi ya dawa, madawa ya kulevya au kemikali, na kadhalika.

NAMNA YA KUKABILIANA NA SHINIKIZO LA DAMU

 1) kula lishe bora na chakula kusichokuwa na mafuta mengi, na pia chenye madini ya potassium .
 2) Kufanya mazoezi mara kwa mara, angalau nusu saa kwa siku.
 3) Kuacha kuvuta sigara na kunywa pombe kwa wale wenye tabia hizo.
 4) Kupunguza utumiaji wa chumvi nyingi katika chakula hasa ya kuongeza mezani (tunapaswa kutotumia zaidi ya gramu 1.5 ya chumvi kwa siku).
5) Kupunguza msongo wa mawazo.
6) Kuhakikisha kuwa tunakuwa na uzito unaotakiwa kiafya kulingana na kimo, na kama tuna uzito uliozidi tunapaswa kupunguza uzito huo ili uwe katika kiwango kinachotakiwa na
7) Kula samaki au kutumia mafuta ya samaki ambayo husaidia kupunguza shinikizo la damu, kwa wenye shinikizo la damu

0 comments:

Post a Comment