Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, April 4, 2014

SABABU ZA KUTOKA HARUFU MBAYA UKENI NA NAMNA YA KUJIKINGA

Wanawake na watu wengi huzani kuwa harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchavu na kutojisafisha vizuri… Matokeo yake huongeza jitihada katika kujisafisha bila mafanikio ya kuondokana na tatizo hili… Kihalisi, badala kusuluhisha, unapojisafisha zaidi ni unaongeza tatizo badala ya kutatua… Japokuwa ni kweli mara nyingine inaweza ikawa ni sababu ya uchafu… Ila mimi naamini walio wengi huwa wanazingatia usafi… Ndo maana nimeona leo tupeane mawazo juu ya tatizo hili, na kujua namna ya kujikinga

Dk. Fadhili Emily wa Fadhaget Sanitarium Clinic

VISABABISHI

i. Bacteria
Tatizo hili husababishwa na Bakteria kwa asilimia kubwa. Kwa asili, ukeni huishi jamii ya bacteria waitwao Lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingila ya uke kuwa katika hali nzuri. Kutokana na njia mbaya za kusafisha uke, hasa kujisafisha kupindukia, ama kwa kutumia sabuni zenye dawa, husababisha bacteria hawa kufa kwa wingi na mahala pake kuchukuliwa na aina zingine za bacteria ambao huzaana kwa wingi na kusababisha tatizo hili.

Pia kwa wale wanaojamiiana kinyume na maumbile, kuna hatari ya kuhamishia bacteria wanaoishi kwenye njia ya haja kubwa na kuwaamishia ukeni ambapo watazaliana na kukuletea madhala haya.

ii. Kuvu(fungus)
Hii mara nyingi huambatana na uchafu mzito utokao ukeni mfano wa maziwa mgando(mtindi)
iii. Magonjwa ya zinaa(STIs)
Kwa asilimia kubwa husababisha na Chlamyidia na kisonono(gonorrhoea). Yote mawili hutibika kirahisi, ila husababisha madhala makubwa zaidi yasipotibiwa kwa wakati. Tukio baya ni kuwa mwanamke anaweza akawa na magonjwa haya na asione dalili yoyote. Ila mara nyingine mwanamke anaweza kujisikia maumivu anapokojoa, na mara nyingine mkojo unakuwa kama una ukungu, vikiambatana na harufu mbaya.
iv. Maambukizi ya via vya uzazi vilivyo ndani ya nyonga[Pelvic Inflammatory Diseases(PID)]
Hii husababishwa na bacteria waambukizwao kwa njia ya ngono wanapofanikiwa kufika kwenye tumbo la uzazi na hata pia mirija ya mimba na hata kokwa(ovaries), hasa chlamydia. Mara nyingi mwanamke anaweza asijisikie chochote hadi pale atakapojisikia maumivu yasiyokwisha ya tumbo(chini ya kitovu), au itakapoingiliana na utungaji wa mimba. Na kama atajisikia, mara nyingi huwa ni maumivu ya nyonga, harufu mbaya, uchafu mzito ukeni, homa, maumivu wakai wa kukojoa na hata maumivu wakati wa kujamiiana.
Tatizo hili lisipotibiwa mapema laweza kusababisha utasa, ama mimba kutunga nje ya mji wa mimba.
v. Kansa ya uke na kansa ya shingo ya kizazi
Asilimia chache sana ya wanawake inaweza ikawa ni kutokana na kansa ya shingo ya kizazi ama ya uke. Hapa ndipo inapoonyesha kuwa tatizo hili siyo la kufumbia macho, na umuhimu wa kuwahi kwa wataalam wa tiba kwa uchunguzi wa mapema na kabla tatizo halijawa kubwa.
vi. Uchafu
Usipokuwa msafi kwa kiwango kikubwa utakuwa unakaribisha wadudu kuzaliana na kukuletea madhala. Pia unatakiwa kuwa makini wakati wa hedhi, na pia uchaguzi wa pedi, kwani kuna pedi ambazo zina kemikali za kukata harufu zinaweza kukudhulu.
JINSI YA KUJIKINGA
• Usiwe unaosha ukeni kupita kiasi kwani husababisha kuondoa bacteria wa asili wa ukeni(Lactobacilli) na kukaribisha bacteria wenye madhala.

• Pia epuka sabuni zenye dawa(antibacterial soap) usafishapo ukeni, kwani hii pia huua bacteria wa asili wa ukeni.

• Hii haimaanishi usiwe unasafisha ukeni. Usafi ni muhimu, kwani uchafu pia hukaribisha vimelea vya magonjwa.

• Kama tatizo limeshajitokeza, wahi haraka kwa wataalam wa tiba wakufanyie uchunguzi na kujua ni kipi kati ya vilivyotajwa hapo juu kilichosababisha. Daktari atakuchunguza na kujua kama ni bacteria, fungus ama ni dalili za awali za kansa na kuchukua hatua mapema kuepusha madhala zaidi.

• Kumbuka kujisafisha kupindukia si suluhisho kama tatizo limeshajitokea, kwani kunaweza kuzidisha tatizo badala ya kusuluhisha.

0 comments:

Post a Comment