Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, February 25, 2015

WATU WATANO WANUSURIKA KIFO AJALINI MWANZA



Muonekano wa mbele wa gari hilo lililopata ajali.

Muonekano wa chini ya gari baada ya kupinduka.




Matofali yaliyokuwa kwenye gari hilo yakiwa yamemwagika chini.

WATU watano (5) wamenusurika kifo ajalini baada ya gari walilokuwa wakisafirishia matofali kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara kisha kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni katika Kijiji cha Ng’ombe wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza ambapo gari hilo aina ya Fuso lenye namba za usajili T726BMY mali ya Sanne Shimbe, lilikuwa likiendeshwa na tajiri huyo.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari hilo lilikuwa kasi, tairi ikapasuka hivyo gari likapoteza uelekeo na kuacha barabara kisha kupinduka.

“Gari lilikuwa kasi hivyo baada ya tairi kupasuka lilitoka barabarani na kuingia kwenye matuta ya viazi vitamu likakwama ndipo likapinduka,” alisema shuhuda.
Kwa upande wake dereva Shimbe, alisema baada ya tairi kupasuka alijitahidi kulizuia gari hilo lisianguke lakini ilishindikana. “Nilijitahidi kuliweka sawa gari barabarani baada ya tairi kupasuka lakini ilishindikana kabisa ndio likatoka barabarani na kupinduka lakini nashukuru Mungu tumetoka wazima.
“Tulikuwa watano, mmoja wetu ndiyo ameumia mguu na ameshapelekwa hospitali, anaendelea vizuri, sisi wengine hatukupata majeraha,” alisema Shimbe.

0 comments:

Post a Comment