Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, February 18, 2015

TBS, MMETEKETEZA U-FRESH NI SAWA, VIPI AFYA ZA WALAJI?




NA Gabriel Ng’osha
FEBRUARI 12 mwaka huu, vyombo vya habari mbalimbali vya hapa nchini viliripoti kuwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza juisi feki aina ya U Fresh zenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 10 ambazo zilikuwa zimetengenezwa chini ya kiwango.

Binafsi nilisikitika sana baada ya kuisikia habari hiyo, na kujiuliza mwenyewe bila kupata jibu, mbona bidhaa hiyo inayodaiwa kuwa ni feki, iko sokoni kwa muda mrefu sasa na walaji wakiendelea kuitumia, hasa watoto wadogo.

Sehemu ya juice zilizoteketezwa.

Nadiriki kusema kuwa sekta husika za ulinzi wa afya za Watazania ambao ni walaji wa bidhaa hizo, ni wazembe, wasio na hofu ya Mungu, hawana uzalendo, wala rushwa na si watu wema kwa afya za Watanzania wenzao.

Yapo maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuteketeza bidhaa hizo ambazo, thamani halisi ya bidhaa iliyoteketezwa ni takribani milioni 10, na katika hali ya kawaida juisi hiyo ilikuwa inauzwa kwa sh.100 kwa kila pakti moja.


Mamlaka ya chakula na dawa TFDA

Na kwa hesabu ya haraka haraka pekti hizo zilikuwa 100,000, Je, ni pakti ngapi zilizoingizwa sokoni na kuathiri walaji? Kuna uwezekano wa kila pakti moja ya juisi feki kuliwa na watoto wawili mpaka watatu. Je ni watoto wangapi mpaka sasa wameathiriwa na juisi hiyo? Na kwa kiwango gani cha madhara wamepata walaji hao? Na vipi kuhusu serikali inachukua hatua gani kwa viongozi wazembe katika idara hiyo ya ukaguzi?

Hivi kweli inaiingia akilini kuiteketeza bidhaa ambayo walaji wake wameshaathirika na juisi hiyo, mlikuwa wapi kudhibiti mwanzoni wakati bidhaa hiyo kabla haijaingia sokoni?. Je, afya za Watanzania mnazifikiriaje kama wadau mlioaminiwa katika kukagua viwango mbalimbali vya bidhaa.

Naomba ninukuu mmoja wa maofisa wa TBS alivyosema katika mahojiano na chombo cha habari “Sisi wenyewe (TBS) tutafuatilia ili kujua kama juisi hizo zimeondolewa sokoni na endapo tutazikuta tutaziondoa,” alisema Andusamile.

Kwa maneno hayo napenda kuuliza maswali kwa TBS na pia kwa ofisa huyo, nini kazi yenu kama wakaguzi wa viwango? Ni kukagua bidhaa ambazo hazijaingia sokoni na kuleta madhara au kukagua bidhaa iliyokwisha leta madhara?.


Maafisa wa TBS wakikagua bidhaa.

Kama mnaweza kutembelea masokoni kuangalia kama juisi hizo zimetolewa, kwanini msiweze kuzuia zisiingie kabisa sokoni?Ni kipi mnachokiweza kama wakaguzi?, Ni yapi mnayofanya tuamini mnalipwa mshahara kihalali na siyo kuwaibia Watanzania ambao kila bidhaa wanakatwa kodi zao?.

Hata kama bidhaa hizi zingekuwa zinazalishwa nje ya nchi bado katika mipaka yetu kuna zaidi ya taasisi tano zinazodhibiti mambo yasiyo sahihi katika bidhaa zinazoingia na kutoka.
Hata kama hamna uzalendo na Watanzania kwasababu hamjatoka nao tumbo moja, Vipi? kuhusu walaji wengine.

Enzi za Mwalimu Julius Nyerere kulikuwa na kauli ya mtoto wa mwenzio ni wako, lakini kwa sasa mtoto wako ni wako tu, wa mwengine hakuhusu. Ngoja niwageukie pia na nyinyi Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) nini kazi zenu katika kuwasidia watanzania ambao hawana utaalamu na vipimo vya kupima kila bidhaa wanayokutananayo sokoni? Uwajibikaji wenu uko wapi kama Watanzania milioni 40 wamewaamini mzilinde afya zao?
TBS Mmeteketeza sawa, hawadhuriki watoto wetu tu hata wenu pia.

0 comments:

Post a Comment