Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, March 4, 2015

SHILOLE ATIA AIBU MSIBA WA KOMBA

IMELDA MTEMA/Amani
MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepondwa vibaya katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba, baada ya kuvaa kigauni kilichombana na kumuonyesha maungo yake ya mwili mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.


Mwanamuziki wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba pamoja na wasanii wenzake kwenye msiba wa Komba.

Baadhi ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta jijini Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo kujitokeza mbele na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni alichovaa bi’dada huyo.

“ Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo tofauti na wenzake ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri maumbo yao, kwa nini yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye alikuwemo kwenye maombolezo.

Paparazi wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza kuhusiana na hilo alisema hakuvaa vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na umbo la mwili wake.

0 comments:

Post a Comment