Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, March 17, 2015

SYLVESTRE MARSH AAGWA JIJINI DAR



Padre akiongoza ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh.

Waombolezaji wakifuatilia ibada ya kumuaga Marsh katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Michezo ya Championi, Saleh Ally akiaga mwili wa kocha Marsh.



Wadau mbalimbali wakiuaga mwili wa Sylvestre Marsh.


Mwili wa Marsh ukitolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mapaparazi wakichukua matukio wakati wa zoezi hilo.


Mwili wa Marsh ukiwa tayari kupelekwa kwenye gari.

ALIYEKUWA kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh, ameagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Marsh aliyefariki dunia jana, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua maradhi ya saratani ya koo kwa muda mrefu.

Awali alilazwa hapo akapata nafuu na kupelekwa kwao Mwanza, lakini wiki iliyopita alirudishwa tena na ndipo umauti ulipomkuta.

Mwili wa Marsh unatarajiwa kusafirishwa kuelekea mkoani Mwanza ambapo maziko yatafanyika.

Mwenyeji Mungu ailaze roho ya marehemu Marsh mahali pema peponi. AMEN

(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)

0 comments:

Post a Comment