Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, March 29, 2015

KANISA LA GOSHENI ENTERNATIONAL MINISTRY LA AZIMISHA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA HUDUMA

Leo katika kanisa la Gosheni Enternational Ministry lililoko Kimara Jijini Dar es Salaam wamesherekea mwaka mmoja wa huduma ya injri Tanzania Tangu kuanzishwa kwake. kanisa hilo lilianza kwa huduma ya kinamama sita mpaka sasa lina zaidi ya Wahumini 50 wakiwemo wamama ,vijana ,wanaume na watoto likiwa na lengo la kusambaa Tanzania nzima na baadae kupanuka katika nchi nyingine Afrika na hata ughaibuni. Akiongea na blog hii kanisani Mchungaji...

Wednesday, March 25, 2015

MUME ALIVYOMFANYIA UKATILI MKEWE

Na Hamida Hassan HUU ni ukatili uliopitiliza! Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Neema Mwita, anateseka katika Hospitali ya Mkoa wa Mara kufuatia jereha kubwa alilopata baada ya mumewe aliyemtaja kwa jina la Juma Mwita kummwagia uji wa moto kisa kikiwa ni kuchuma mahindi shambani bila ridhaa ya mumewe huyo.Akizungumza na Uwazi huku akimwaga machozi kila wakati, mwanamke huyo alisema siku ya tukio, yeye na mumewe walikuwa kazini na mwanaume...

HAYA NDIYO MAAJABU YAKE MTOTO ALIYENUSURIKA KWA MKONO WA MUNGU

Na Haruni Sanchawa MTOTO Jacqueline Lepenza, aliyenusurika katika ajali mbaya ya basi lililogongana na lori huko Mafinga mkoani Iringa wiki mbili zilizopita, ameripotiwa kuwa na maajabu baada ya baba yake mzazi kujitokeza na kusimulia, Uwazi linakutaarifu. Jacqueline Lepenza, akiwa na baba'ke. Willy Lupenza, baba mzazi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, alisema marehemu mke wake, Anjela Osward (35) (pichani) alikuwa amekwenda nyumbani...

MAAMBUKIZI YA FANGASI SEHEMU ZA SIRI -3

WIKI iliyopita tulieleza madhara ya fangasi zehemu ya siri na jinsi ugonjwa huo unavyosumbua wanawake. Leo tunaendelea kuelezea fangasi sehemu za siri wanavyosumbua na tuliahidi kwamba tutaeleza tiba yake. Baada ya kueleza mengi kuhusiana na ugonjwa huu leo tutaeleza matibabu yake ambayo huusisha dawa za kutibu fangasi (antifungal drugs) kama vile dawa za kupaka za Topical Clotrimazole, Topical Nystatin, Fluconazole au Topical Ketoconazole. Wagonjwa...

NDEGE YA UJERUMANI YAANGUKA IKIWA NA WATU 150

Ndege ya shirika la ndege la Germanwing inayofanana na ile iliyoanguka. NDEGE ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa. Mchoro ukionyesha eneo ambalo ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada. Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 142 na wahudumu sita ikitokea jijini Barcelona nchini Uhispania kuelekea Duesseldorf, Ujerumani. Ubao wa kuonyesha ndege zilizowasili kwenye uwanja...

KIFUA KIKUU: UGONJWA UNAOUA ZAIDI YA WATU MILIONI 1 DUNIANI KILA MWAKA

Mgonjwa wa kifua kikuu akipatiwa matibabu. KWA Tanzania, watu 120,191 hukisiwa kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka, hii ni kutokana na taarifa ya Shirika la USAID ya mwaka 2007 na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kifua kikuu ni 32,000 kila mwaka hapa nchini Tanzania. Muonekano wa mapafu ya binadamu yaliyoathirika kwa TB. Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonyesha kuwa Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa sana...

ANGELINA JOLIE AFANYIWA UPASUAJI, ATOLEWA OVARI, MIRIJA YA UZAZI

Angelina Jolie. MWIGIZAJI wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie amelazimika kutoa ovari zake pamoja na mirija ya uzazi baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi. Angelina Jolie, mumewe Brad Pitt wakiwa na watoto wao. Staa huyo maarufu wa Hollywood amelidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa viungo hivyo wiki iliyopita katika upasuaji wa dharura. "Upasuaji...

Sunday, March 22, 2015

WASAFIRI RAIA WA CAMEROON WATEKWA NYARA

Wasafiri kadhaa raia wa Cameroon wameripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana karibu na mpaka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Duru za kuaminika zimeripoti kuwa, watu hao 15 wametekwa nyara na watu wenye silaha wa kundi linaloongozwa na mtu mmoja anayetambulika kwa jina la Abdoulaye Miskine, huko kaskazini mashariki mwa Cameroon karibu na mpaka wa pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Chanzo kimoja cha usalama nchini Cameroon kimeeleza kuwa, wasafiri...

IS YAKIRI KUSHAMBULIA MISIKITI YEMEN

Majeruhi wakiokolewa baada ya shambulizi lililotekelezwa na Kundi la wapiganaji wa IS katika misikiti ya Yemen. Kundi la Islamic State linasema kuwa wapiganaji wake waliendesha mashambulizi ya kujitoa mhanga kwenye misikiti miwili nchini Yemen ambapo zaidi ya watu 130 waliuawa. Washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walilenga waumini kwenye mji mkuu Sanaa wakati wa maombi ya Ijumaa. Maeneo hayo mawili hutumiwa na waumini wanaowaunga mkono waasi...

WATU WAPATAO 70 WANAOSADIKIWA KUUAWA NA BOKO HARAM WAGUNDULIKA DAMASAK, NIGERIA

Askari wa Chad na Niger wakiwa Damasak. Makumi ya miili ya watu wanaosadikiwa kuuawa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri wa Boko Haram, imegunduliwa katika Mji wa Damasak uliopo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Taarifa zinaeleza kuwa, miili hiyo ya watu 70 ambayo mingi kati yake imekutwa ikiwa imekatwa vichwa, imegunduliwa na askari wa Chad na Niger katika mji huo wa Damasak nchini humo. Tayari uchunguzi umeanzishwa kwa lengo la kuwatambua...

MISS TANZANIA AFUNGUA MFUKO MAALUM KUWASADIA WATOTO WANAOZALIWA KABLA YA SIKU ZAO

Dorice Molle (katikati) akiwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Thabit Kombo. Hapa wakizindua rasmi mfuko wa kusaidia watoto ambao ni njiti (Premature). Mkurugenzi wa Shindano la Miss Tanzania, Hashimu Lundenga akiteta jambo na Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu. Mama mzazi wa mrembo huyo na kaka yake ambao nao walihudhuria hafla hiyo. Kada wa chama CCM, Chrisant Mzindakaya naye alikuwepo. Dorice akizungumza jambo na kutoa shukrani. Baadhi ya wageni...

Wednesday, March 18, 2015

MWANAO WA KUMZAA UNAWEZA KUMTESA HIVI?

HARUNI SANCHAWA MWANAMKE mmoja mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Violet Manyondo (40) anadaiwa kumtesa na kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto wake wa kumzaa, anayejulikana kwa jina la David (14).David ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule moja ya msingi iliyopo Mzambarauni, Dar kwa sasa haendi shule kutokana na majereha aliyonayo kiasi cha kuwaliza majirani. Mtoto David akiwa na majeraha mwilini aliyosababishiwa na mama...

DENTI MWENZAKE LULU ACHOMWA KISU, AFARIKI

WAANDISHI WETU, DAR CHAMIWA Adamu (23), kijana ambaye ni mkazi wa Kilimahewa- Manzese jijini Dar, ameuawa kwa kuchomwa kisu cha shingo na mtu aliyetambulika kwa jina moja la Mpelu kisa kikidaiwa ni shilingi mia mbili tu! Marehemu Chamiwa Adamu enzi za uhai wake. Marehemu Chamiwa (pichani)alikuwa mwanafunzi mwenzake na staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye Chuo cha Magogoni, Dar. Tukio la Chamiwa kuchomwa kisu lilijiri saa 11...