Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, May 18, 2015

UVIMBE KATIKA VIFUKO VYA MAYAI (OVARIAN CYST)




Hii ni hali ya mkusanyiko wa maji kuzunguka kifuko cha mayai. Ni ngozi laini na nyepesi juu ya kifuko cha mayai. Kifuko cha mayai huwa kinachipua vifuko vidogovidogo ‘Follicles’ na endapo follicles hizi zitakuwa na ukubwa zaidi ya sentimeta mbili, basi ndiyo huitwa Ovarian Cyst.

Uvimbe unaweza kuwa na ukubwa kuanzia saizi ya punje ya njegere hadi saizi ya ukubwa wa chungwa. Aina nyingi ya uvimbe huu huwa hauumi na hauwi saratani na huweza kutokea na kupotea ingawa unaweza kuwa mkubwa zaidi.

Ovarian Cyst huwatokea wanawake wa umri wote kuanzia watoto wachanga hadi mwanamke anapofikisha umri wa kuzaa. Uvimbe pia hutokea hata kwa wanawake waliokoma hedhi. Baadhi ya aina hizi za uvimbe huleta matatizo mfano kuvuja damu na maumivu makali au kugeuka kuwa kansa.

Endapo uvimbe utakuwa mkubwa zaidi ya sentimeta tano, basi upasuaji utafanyika kuuondoa lakini ukiwa chini ya hapo unaweza kutibika kwa dawa. Aina za uvimbe wa Ovarian Cyst Uvimbe huu unaweza kutokea kufuatana na mzunguko wa hedhi na huitwa ‘functional cyst’ ambapo huu wa Ovarian Cyst unaweza kuwa mkubwa endapo utakuwa na zaidi ya sentimeta tano na kuwa mkubwa zaidi hadi kufikia ukubwa hadi usawa wa kitovu.

Uvimbe ambao hutokea wakati wa hedhi kitaalamu huitwa functional cyst na umegawanyika kwenye makundi matatu ambayo ni Follicular Cyst, Corpus Luteum Cyst na Thecal Cyst. Aina hizi za uvimbe huwa hazizidi ukubwa wa sentimeta tatu na wastani hukaa kwa kati ya siku tano hadi tisa na hupotea wenyewe. Aina hizi zinatokea kufuatana na mfumo wa hedhi uitwao Functional na uvimbe ambao hutokea bila ya uhusiano na hedhi huitwa Non Functional ambao kwa vyovyote huhitaji uchunguzi wa kina.

Dalili za uvimbe
Uvimbe unaowatokea watoto wadogo wa kike kabla ya kuvunja ungo huitwa Juvenile Ovarian Cyst na umegawanyika katika makundi tofauti. Kama tulivyosema huwa mkubwa hadi kufikia usawa wa kitovu na kumsababishia mtoto alalamike kuumwa na tumbo chini ya kitovu mara kwa mara.

Maumivu haya huwa makali hata kabla uvimbe haujawa mkubwa. Maumivu pia humpata hata mwanamke mwenye uvimbe ambaye tayari ameshakua au ameshavunja ungo. Hapa mwanamke hulalamika maumivu ya mara kwa mara ya tumbo chini ya kitovu na hushika hadi kiuno na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

0 comments:

Post a Comment