Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, May 11, 2015

MAFURIKO YAWALIZA MASTAA

Gladness Mallya
KUTOKANA na mvua kubwa iliyonyesha na inayoendelea jijini Dar ambayo imesababisha mafuriko kwenye majumba ya watu na maji kujaa barabarani hivyo magari kushindwa kupita, baadhi ya mastaa Bongo, wamejikuta wakilizwa na hali hiyo kwani imewaathiri katika maisha yao ya kawaida na kwenye kazi zao.

Adha ya mafuriko jijini Dar.

Wakizungumza na gazeti hili juu ya majanga hayo ya mafuriko yaliyowakumba hasa watu waishio mabondeni, mastaa hao walikuwa na haya ya kusema:

WASTARA JUMA:
“Mafuriko yameniathiri kwani niko karibu na Mto Msimbazi (nyumbani kwake Tabata) hivyo hata kutoka nyumbani naogopa kwa sababu ya watoto. Nyumba ninayoishi kuna mfereji niliochimba nje, ukijaa maji yanaingia kwenye vyoo ndani, shida tupu.”

AUNT EZEKIEL:
“Niko tu ndani (Mwananyamala) siwezi hata kutoka kwenda popote kwa sababu maji yamejaa kila sehemu, nimesimamisha shughuli zangu kwa sababu barabara zenyewe hazipitiki, ukweli hii mvua imeathiri sana.”



YOBNESH YUSUF ‘BATULI’:
“Ukweli naipongeza sana serikali kwa miundombinu mibaya, bungeni kila mwaka wa bajeti zinapitishwa mamilioni ya fedha lakini miundombinu mibovu, mafuriko kila sehemu nyumbani (anaishi maeneo ya Sinza) ni shida.

KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
“Namshukuru Mungu nyumba yangu ipo mlimani (anaishi Jet-Lumo) maji hayajaingia ndani lakini hali ni mbaya kwani siwezi kutoka kwenda kwenye shughuli zangu, mipango yote imekufa nashinda ndani tu na familia.“Watoto hawajaenda shule, walimu walitupigia simu wakasema wasiende kutokana na hali halisi ya mafuriko.”

AUNT EZEKIEL.

MAYASA MRISHO ‘MAYA’:
“Huku ninakoishi (Msasani) maji yamejaa kweli kila sehemu, hakuna pa kupita huko kwa mama yangu Magomeni sijui itakuwaje maana ndiyo zaidi, serikali inatakiwa iliangalie suala hili na kulitatua kwani hii yote inatokana na miundombinu mibovu.”

0 comments:

Post a Comment