Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, May 27, 2015

DAKTARI: MBONI MASIMBA ILIKUWA AFE




Imelda mtema
Mtangazaji mahiri wa Kipindi cha The Mboni Show kinachorushwa kupitia Televisheni ya Taifa ya TBC1, Mboni Masimba, amejikuta akiangua kilio kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar, alipotembelea wodi ya wazazi na kusimulia jinsi ambavyo daktari alimweleza kuwa ilikuwa kiduchu tu afe wakati wa kujifungua hivi karibuni.


Mtangazaji mahiri wa Kipindi cha The Mboni Show, Mboni Masimba akihojiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akiwa wodini hapo juzikati, Mboni ambaye pamoja na timu yake walikwenda kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya msaada kwa akina mama ambao wapo kwenye wodi hiyo, alisema kuwa hospitali ambayo ni ya uhakika ni Muhimbili pekee kwani ndiyo walionusuru uhai wake.

“Daktari alinieleza kuwa mimi nilikuwa ni wa kufa jamani hapa ndipo niliporejeshewa uhai wangu tena japokuwa nilijifungulia hospitali nyingine lakini huko kote walishindwa, hapa ndipo walinitibu pekee na niliweka ahadi kuwa nitarudi kwa ajili ya kutoa kwa wengine,” alisema Mboni.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Uzazi, Dk. Mathew Kalianga alisema kuwa ugonjwa uliompata Mboni kitaalam unaitwa Pulmonary Embolism ambapo mara nyingi watu wanaopata ugonjwa huo ni asilimia tano tu kati ya mia ndiyo wanapona hivyo Mboni ni mmoja aliyebahatika.

Pulmonary Embolism ni ugonjwa wa Kuganda kwa damu ambao husababisha mshipa mkubwa unaosafirisha damu na hewa kwenda kwenye mapafu kuziba. Hali hiyo huweza kusababisha mtu kufariki dunia ghafla. Ndiyo uliomuua mwanamuziki wa Nigeria marehemu Goldie.

Mboni aliyesindikizwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alitoa msaada wa mashuka, viti vya matairi na vingine vingi vinavyohitajika wodini hapo.

SOURCE: Global Publisher

0 comments:

Post a Comment