Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, May 11, 2015

BOKO HARAM YASHAMBULIA CHUO NIGERIA, 12 WAJERUHIWA VIBAYA



Shambulio la Boko Haram nchini Nigeria.

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram, amefanya shambulizi la kujitoa mhanga katika Chuo kimoja cha Masomo ya Uongozi wa Biashara nchini Nigeria na kuwajeruhi wanafunzi kadhaa.

Tukio hilo limetokea jana Mei 8, 2015 baada ya mtu huyo kuvuka geti na kuingia ndani ya chuo hicho na kutekeleza shambulio hilo kwa kufyatua risasi kisha kujilipua kwa mabomu.

Madhara ya shambulio la Boko Haram nchini Nigeria.

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimeripoti kuwa, shambulizi hilo lilifanyika katika Chuo kimoja cha Masomo ya Uongozi wa Biashara kilichopo mji wa Potiskum katika jimbo la Yobe Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Katika shambulio hilo, watu 12 wanasemekana kujeruhiwa wakiwemo wanafunzi wa chuo hicho na wengine wakiwa katika hali mbaya.

Hii ni katika hali ambayo mtu mwingine aliyekuwa amejifunga mabomu amepoteza maisha baada ya mabomu hayo kumripukia kabla ya kufika eneo alilokusudia kufanya shambulio.

“Tumewaona watu 12 waliojeruhiwa vibaya na shambulio hilo ambao wamepelekwa hospitali kwa matibabu”.

“Tulikuwa ndiyo tumeingia darasani kuanza vipindi, tukasikia milio ya bunduki kutoka kwenye usawa wa geti la kuingia chuoni, hapo tukagundua kuwa tumevamiwa ndipo kila mtu akaanza kukimbia kutoka darasani ili kunusuru maisha yake” Tijjani Musa, alisema.

Ingawa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mashambulizi hayo, lakini polisi ya Nigeria imelitaja kundi la kigaidi la Boko Haram kuwa ndilo linalohusika.

Watafiti wa mambo wanayataja mashambulizi hayo kuwa ni juhudi za mwisho za Boko Haram katika kuonesha uwepo wake, baada ya kuzidiwa nguvu na jeshi la Nigeria hivyo kuyakimbia maeneo mengi liliyokuwa likiyadhibiti.

CHANZO: MTANDAO WA PULSE.NG

0 comments:

Post a Comment