Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, May 24, 2015

MBUNGE WA SOMALIA, YUSUF DIRIR AUAWA KATIKA SHAMBULIO MOGADISHU




Gari alilokuwemo Yusuf Dirir.

MBUNGE wa Somalia, Yusuf Dirir ameuawa kwa kupigwa risasi katika Mji wa Mogadishu jana.
Wanausalama wameeleza kuwa Yusuf Dirir aliuawa baada ya gari lake kushambuliwa na wanamgambo wanaodhaniwa kuwa wa Kundi la Al Shabaab.

Wapiganaji wa Al Shabaab.

Wafanyakazi wengine watatu wa Wizara ya Usafirishaji nao pia waliuawa katika shambulio lingine lililotokea jana.
Takribani wabunge watano waliuawa na Kundi la Al Shabaab mwaka jana huku kundi hilo likidai kuendeleza mauaji dhidi ya wabunge.

Kundi hilo jana Jumamosi lilipambana na vikosi vya majeshi ya serikali katika Wilaya ya Awdigle na Kijiji cha Mubarak kusini mwa Mji wa Mogadishu.

Katika mapigano hayo, takribani watu 17 wameripotiwa kupoteza maisha.

0 comments:

Post a Comment