Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, May 27, 2015

LIFAHAMU TATIZO LA UVIMBE KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA (BAWASIRI)-2




Wiki iliyopita tulianza kupeana elimu juu ya tatizo la kuota kijinyama katika njia ya haja kubwa (bawasiri). Tuliangalia chanzo cha ugonjwa huu na nikawapa ushauri kwamba ukiona una tatizo hilo ni vema ukawa huru maana ni ugonjwa wa kawaida na unatibika kama magonjwa mengine. Hivyo ni vema ukawahi katika vituo vya tiba ili upate matibabu mapema na kuepukana na adha za ugonjwa husika. Leo tutaangalia dalili za ugonjwa huu wa bawasiri.

Kwa kuwa ugonjwa huu hutokea katika eneo ambalo humfanya mgonjwa ajisikie aibu na dalili zake ni mgonjwa mwenyewe ndiye anaweza kuziona na asijisikie vibaya kuwaeleza wataalamu wa afya ili apewe matibabu mara moja. Dalili za ugonjwa huu ni kama zifuatazo;

Kwanza kabisa ni maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Wengi hupata maumivu makali sana wakati wa kutoa haja kubwa. Na wengine mpaka wanatokwa na machozi kwa maumivu lakini wanakaa kimya wanaona kama ni hali ya msimu itakwisha. Napenda kukujulisha kuwa hali hiyo si ya kawaida ni dalili ya ugonjwa huu wa bawasiri ni vema uonapo hali hiyo wahi katika vituo vya tiba.

Kinyesi kuwa na harufu ya damu wakati wa kujisaidia. Niwakumbushe kuwa unapoona damu kwenye kinyesi ni dalili kuwa kuna tatizo katika njia yako ya haja kubwa hivyo unapaswa kuchuka hatua za haraka kujua sababu ya damu hiyo kutoka.

Wakati mwingine kutokana na tatizo hili kushambulia njia ya haja kubwa kuna wakati mgonjwa atashindwa kuzuia haja yake na hivyo haja kuvuja. Hilo si jambo la kawaida ni viashiria vya hatari katika mfumo wa haja kubwa.

1 comment: