Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Saturday, April 25, 2015

WEMA AKUBALI WAGANGA 26 KUMTIBU

Musa mateja
KUFUATIA tatizo la kushindwa kupata ujauzito alilonalo msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu, hivi karibuni waganga wapatao 26 kutoka sehemu mbalimbali nchini walijitokeza na kuomba kuunganishwa na staa huyo ili wamtibu.

Msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu.
Waganga hao wa tiba asilia pamoja na madaktari kutoka hospitali mbalimbali kwa nyakati tofauti walililipigia simu gazeti hili na kueleza kuwa, wanashangaa kuona Wema anakosa amani wakati wao wanaweza kumtibu na kuweza kuitwa mama kama wenzake.

“Unajua wapo wanawake ambao wanakosa amani kwa mambo ambayo hawastahili, hili la Wema kutopata mtoto linatibika, mpeni namba yangu kisha anitafute,” alisema mmoja wa wataalam hao aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Katika kujua Wema anapokeaje ofa aliyopewa na waganga hao, alitafutwa na alipopatikana alikubali mara moja kutibiwa tatizo alilonalo lakini akatoa angalizo.

“Kuna watu wengi sana ukiacha ambao wamejitokeza kwenu, mimi nina meseji zaidi ya 400 ambazo nimetumiwa kwenye namba yangu ya WhatsApp na simu kibao nimepigiwa watu wakijitolea kuja kushughulikia tatizo langu, kiukweli kabisa nipo tayari.

“Lakini ni vizuri wakati naanza kutibiwa tayari nikawa na mwenza wangu ambaye tutakuwa tumekubaliana na pale tatizo litakapoisha, iwe rahisi kuzaa mara moja,” alisema Wema.

0 comments:

Post a Comment