Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, April 26, 2015

MJAMZITO ATIBUA ONESHO LA YAMOTO BAND


Richard Bukos na Issa Mnally
Dada mmoja aliyedaiwa kuwa mjamzito usiku wa Ijumaa iliyopita alizua tafrani na kusababisha onesho la Yamoto Band kusimamishwa baada ya kuvamia jukwaa na kufanya ndivyo sivyo huku kitumbo chake kikiwa kimejichomoza kiuchokozi kufuatia kuachwa wazi.

Kisa hicho cha kushangaza kilitokea ndani ya Ukumbi wa White House uliopo Kimara jijini Dar ambapo Yamoto Band kwa kushirikiana na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ walikuwa wakifanya makamuzi ya pamoja.

Katika tukio hilo, dada huyo na mwenzake walikuwa wakilivamia jukwaa na kuwasonga wanamuziki ambapo mabaunsa waliposhindwa kuwadhibiti waliamua kuzima muziki na kuwasihi wateremke chini wakatii.

0 comments:

Post a Comment