Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, April 8, 2015

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UNAOTOKANA NA KISUKARI (DIABETIC NEPHROPATHY)



Yapo madhara ya ugonjwa wa kisukari katika mwili wa binadamu na mojawapo ni ugonjwa wa figo (Diabetic Nephropathy) pamoja na ukosefu wa nguvu za kiume.Matatizo haya huwapata watu wenye kisukari na hutokea muda mrefu baada ya mtu kugunduliwa kuwa na maradhi ya kisukari.

Tutaeleza baadaye kwa nini wenye ugonjwa wa kisukari wanakuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, lakini leo tuangazie tatizo la figo ambayo ina mamia kwa maelfu ya vijiumbo vidogovidogo viitwavyo nefroni (nephrons). Kazi ya hizi nefroni ni kuchuja damu na kutoa uchafu mwilini mwako kwa njia ya mkojo.

Kwa watu wenye kisukari, nefroni huwa na tabia ya kunyauka, kuzeeka na kuwa na makovu kadiri miaka inavyopita. Baada ya muda fulani, hushindwa kabisa kazi yake ya kuchuja uchafu, matokeo yake protini ambazo kwa kawaida huwa haziwezi kuchujwa, hufyonzwa na kutoka katika mkojo.

Chanzo hasa cha kunyauka na kuzeeka huko au kuwa makovu kwa nefroni hakijulikani, lakini udhibiti mbaya wa sukari husababisha uharibifu wa figo, na madhara huongezeka maradufu kwa watu wenye shinikizo la damu lisilodhibitiwa.

Ifahamike kuwa si kila mwenye kisukari anaweza kupata ugonjwa wa figo lakini watu wengi wenye maradhi haya kwa upande wa wanaume huwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Wagonjwa wa kisukari ambao pia ni wavutaji wa sigara, na wale wenye aina ya kwanza ya kisukari (type 1 Diabetes Mellitus) kilichoanza kabla hawajafika miaka 20, wana hatari kubwa ya kupata matatizo ya figo.

Dalili
Kwa kawaida, mtu mwenye tatizo hili anaweza asioneshe dalili zozote katika miaka ya mwanzo ya ugonjwa. Mara nyingi dalili huanza kujitokeza miaka 5 mpaka 10 baada ya figo kuathirika nazo ni kukosa hamu ya kula, kujihisi uchovu na kwa jumla kutojihisi vizuri. Dalili nyingine ni pamoja na kuumwa kichwa, kichefuchefu na kutapika na kuvimba miguu.

Vipimo
Kwa watu wenye kisukari, wanashauriwa kufanya uchunguzi wa figo zao mara moja kwa mwaka ambapo utachunguzwa kama una dalili zozote zinazoashiria matatizo ya figo. Utapimwa mkojo kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha protini iitwayo albumin au microalbuminuria.

Kuwepo kwa kiasi kingi cha protini katika mkojo ni mojawapo ya dalili za kuwepo kwa tatizo katika figo.Vipimo vingine ni pamoja na kiasi cha Urea Nitrogen katika damu (BUN), kiwango cha creatine katika damu (serum creatinine), kiasi cha protini katika mkojo wa saa 24 (24-hour urine protein), kiasi cha madini ya phosphorus, calcium, bicarbonate, PTH, na potassium katika damu, kiasi cha wingi wa damu (Hemoglobin), na wakati fulani kufanya biopsy ya figo kwa ajili ya uthibitisho wa tatizo

0 comments:

Post a Comment