Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, April 13, 2015

JEURI YA FEDHA: APATA AJALI NA LAMBORGHINI YA MIL 675, ASEMA ATANUNUA NYINGINE KESHO YAKE

Lamborghini Gallardo baada ya kugonga mti na kuparamia vizuizi vya barabarani.

KATIKA kuonyesha jeuri ya fedha, mmiliki mmoja wa gari aina ya Lamborghini Gallardo huko nchini England ametoa mpya baada ya kupata ajali na kuwaambia mashuhuda kuwa kesho yake angenunua gari lingine kama hilo.

Gari hilo la thamani likiwa limeharibika baada ya ajali.

Mmiliki huyo alipata ajali katika eneo la Beaumont Leys, Leicestershire baada ya kugonga mti na kisha kugonga vizuizi vya barabarani.

Katika ajali hiyo, Lamborghini hiyo yenye thamani ya pauni 250,000 sawa na shilingi milioni 676 za Kitanzania ilichomoka tairi moja la nyuma.


Tairi ya nyuma iliyochomoka baada ya ajali.

Baada ya kutokea ajali hiyo, alishuka kijana mdogo ambaye hakufahamika jina lake na kuwaambia mashuhuda wa ajali hiyo, kuwa hakuna tatizo kwa gari hilo kuharibika maana atanunua lingine kesho yake.

0 comments:

Post a Comment