Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, April 12, 2015

MAGWIJI WA TANZANIA WAFUNGWA 2-1


MAGWIJI wa Tanzania wamefungwa magoli 2-1 na Magwiji wa Barcelona katika mechi ya kirafiki iliyopigwa uwanja wa Taifa hapo jana huku msanii Farid kubanda Fid Q na Ambwene Yesaya "AY" wakionesha wazi kuwa ni mashabiki wa klab ya Barcelona wapotinga uwanjani hapo wamevaria jezi za klab hiyo

Bao la kwanza la Barcelona limefungwa na Luis Garcia katika dakika ya 9′ akimalizia mpira wa kona uliochongwa na mkali wao, Mholanzi, Patric Kluivert.
Tanzania walisawazisha dakika ya 44′ kupitia kwa Yusuph Macho.
Barcelona waliandika bao la pili na la ushindi katika dakika ya 86′ kupitia kwa Kluivert aliyefunga kwa mwakwaju wa penalti baada ya beki Mustapha Hoza kumuangusha Kluivert mwenyewe.
Farid Kubanda "Fod Q" na Ambwene Yesaya "AY" wakitizama mtanange huo

Meneja wa Tv51 /Blogger Lonelynzali Na Kichaka wa Azamu Tv tulikuwa pamoja kukujuza matukio

Mchezaji Patrick Kluvert naodha wa timu ya Barcelona na naodha wa Taifa starz wakiwa wamebeba
watoto walemavu wa ngozi ambao ni mmoja ya jambo lililowaleta magwiji hao katika harakati za
kupinga mauaji dhidi ya walemavu wa ngozi

Nahodha Patrick Kluvert Baada ya kuwafunga Taifa stars goli la pili kwa mkwaju wa penati

Kikosi cha Magwiji wa Tanzania kilichokabiliana na Magwiji wa Barcelona

Kikosi cha Magwiji wa   Brcelona  kilichokabiliana na Magwiji wa Tanzania

Nahodha wa timu ya magwiji wa Tanzania wakijipanga Baada ya kufungwa goli la kwanza

Faulo upande wa goli la Magwiji wa Tanzania

.

0 comments:

Post a Comment