Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, April 20, 2015

UGONJWA KWENYE KIBOFU KWA WANAWAKE-2


Mfano ni ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi. Pia wanawake wenye uzito wa zaidi ya kilo 70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata ‘fibroids’ kutokana na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ katika umri huo.

Zamani ‘fibroids’ ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa sababu vidonge hivyo vilikuwa na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen.’ Hivi sasa vidonge hivi vya uzazi wa mpango havina kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ kama ilivyokuwa zamani.

‘Fibroids’ zinatofautishwa kutokana na sehemu ilipotokea. Zipo zinazotokea ndani ya mji wa mimba na zingine zinazotokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba.Karibu asilimia 75 ya wanawake wenye ‘fibroids’ hawajui kama wana ‘fibroids.’ Utambuzi wa dalili za ‘fibroids’ hutegemea ukubwa wake na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia huchangiwa na dalili anazopata mtu. Fibroids’ ndogo iliyo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na ‘fibroids’ kubwa inayoota nje ya kizazi.

DALILI ZA FIBROIDS
Dalili kubwa inayofahamika zaidi ni ile ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na maumivu ya tumbo na damu hiyo huambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida.Dalili nyingine ni kupata maumivu ya kiuno, ugonjwa hubana viungo vingine vya mwili (pressure symptoms) hivyo kupumua kwa shida au kukojoa mara kwa mara au kushindwa kupata choo kikubwa kama kawaida. Nyingine ni pamoja na kutokutunga mimba, au mimba kuharibika na kutoka.

Ni rahisi kwa mtaalamu kugundua ugonjwa huu au uvimbe katika mfuko wa uzazi kwa kumkagua, au kumpima mgonjwa (bimanual examination). Pia huathiri mfumo wa haja ndogo na kubwa na mgonjwa kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogokidogo, kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo, kutopata mimba na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

‘Fibroids’ zaweza kusababisha matatizo kama kuharibu mimba au mwanamke kutoshika mimba kutokana na mirija ya uzazi kubanwa au msukumo unaosababishwa na ‘fibroids’, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus).

Mwanamke anapokuwa mjamzito na pia akawa na ‘fibroids’, mwili huweza kusitisha kupeleka damu kwenye ‘fibroids’ na kuifanya isinyae hivyo kusababisha maumivu makali ya tumbo na kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa na baadaye mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.

Wakati wa kujifungua, kama ‘fibroid’ itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka au ikishindikana, mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliye tumboni.

USHAURI
Dalili zikiwapo na kuhisi unalo tatizo la ‘fibroids’, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo kujua kama una ‘fibroids’ au la. Daktari atafanya vipimo vya ‘Ultrasound’ (mionzi), ‘Hysteroscopy’ (kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke) na ‘Laparosopy’ (upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke).

TIBA
Kuna njia kuu mbili za kutibu ‘fibroids’. Kutumia dawa (drug treatment). Mkusanyiko wa dawa zijulikanzo kama ‘GnRH analogues’ hupunguza kiwango cha ‘oestrogen’ mwilini na hivyo kusababisha ‘fibroid’ kusinyaa. Dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa ‘fibroid’ kwa aslimia 50 pia hupunguza mzunguko wa hedhi.

Matumizi ya dawa za ‘GnRH analogues’ yasizidi miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa baadaye. Mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi,wanawake wengine baada ya wiki chache hujikuta wakirudiwa na ‘fibroids’ ambazo huanza kukua tena na mwanamke huanza kupata hedhi kama awali lakini ikiambatana na maumivu makali. Baadhi ya wanawake huwa hawapati hedhi tena kwa maisha yao yote.

Upasuaji ni njia nyingine ya kutibu ugobnjwa huu na huhusisha mambo yafuatayo: Kuiondoa ‘fibroid’ yenyewe na kuacha kizazi jambo ambalo kitaalamu huitwa myomectomy; kukiondoa kizazi kabisa kitaalamu huitwa hysterectomy na kuzuia damu kwenda kwenye ‘fibroids’ yaani uterine artery embolisation. Pia iko njia ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni zikielekea zilipo ‘fibroids’ kwa ajili ya kuziua kwa kemikali maalumu.

Ugonjwa unapoingia kwenye kibofu cha mkojo huwa ni tatizo kubwa kwa wanaume pia.
Wanaume, hasa wenye umri mkubwa wanaweza wakawa na ugonjwa wa saratani ya ‘prostate’. Ni tezi iliyo kwenye viungo vya uzazi vya wanaume chini ya kibofu panapopitia mrija wa mkojo.

Kazi ya ‘prostate’ ni kudhibiti kibofu na mtiririko wa mkojo lakini pia ni muhimu katika tendo la ndoa kwani humwezesha mwanamume kuwa na nguvu ya kufikia kilele. ‘Prostate’ ya kawaida kwa mwanamume mtu mzima ina ukubwa kama punje ya karanga na ukubwa huu huongezeka kadiri mtu anavyokua. Katika umri wa miaka 40 tezi huanza kutanuka na kadiri inavyotanuka, hubana mrija wa kupitisha mkojo na kufanya mkojo utoke kwa shida na kusababisha tatizo katika tendo la ndoa.

DALILI
Dalili za kwanza za mgonjwa kuwa na tatizo katika kibofu cha mkojo ni kwenda haja ndogo mara kwa mara, hasa usiku na mara nyingine mtu huweza kujikojolea. Pia mkojo hutoka kidogokidogo ama kwa kukatika katika na wakati mwingine mwanamume hupata maumivu wakati wa kukojoa na hata kutoka damu. Maumivu huenea kwenye sehemu za mgongo, kiuno na sehemu za juu ya mapaja na kupunguza uwezo wa tendo la ndoa au kupata maumivu wakati wa kufikia kilele.

Matatizo mengine ni kupata maambukizi ya magonjwa kwenye kibofu, njia ya mkojo na figo na mkojo hubaki kwenye damu na kuwa sumu. Utafiti waonesha kuwa asilimia 25 ya wanaume wenye umri wa miaka 30 na kuendelea wana chembechembe za ‘prostate cancer’.

‘Prostate cancer’ ndio aina kuu ya ‘cancer’ (saratani) inayowashambulia sana wanaume japokuwa inaweza kutibika mgonjwa akiwahi hospitali.

0 comments:

Post a Comment