Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, April 17, 2015

WATU 19 WAFARIKI KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU KAHAMA


Wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo ya kijiji cha Karore, Kata ya Runguya, Tarafa ya Msalala mkoani Kahama.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justus Kamugisha, amesema usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivavamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.

0 comments:

Post a Comment