Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, April 17, 2015

AJALI IMETOKEA JIJINI MBEYA, ZAIDI YA WATU 20 WAMEDAIWA KUPOTEZA MAISHA


Baadhi ya wakazi wa jirani na eneola tukio wakitazama gari lilivyopata ajali kando kando ya mto Kiwira.

Wananchi wa Kiwira wakienda kuangalia ajali hiyo.

Wananchi wa Kiwira wakiangalia baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukia kwenye Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaidi ya watu 20 waliokuwemo kwenye gari hilo wamepoteza Maisha.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, inasemekana kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya Hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea Hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.

Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.

Mungu aziweke mahala pema peponi roho za marehemu hao, AMEN.

0 comments:

Post a Comment