Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, April 13, 2015

MWANZA: MAMA AJIFUNGUA MTOTO, AMTUPA DAMPO

Na Johnson James, GPL / Mwanza

MAMA mmoja mkazi wa kata ya Mkuyuni-Sokoni wilayani Nyamagana jijini Mwanza (jina lake halikufahamika mara moja) amejifungua mtoto wa kiume na kisha kumtupa kwenye shimo la kutupa taka (jalala) eneo a Mkuyuni jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa watoa taarifa kwa viongozi wa serikali aliyetoa sharti la kutotajwa jina lake amesema:

“Mimi ni mfanya usafi hapa Mkuyuni, wakati ninaenda kumwaga uchafu pale dampo nikakuta kitoto kichanga kimetupwa maeneo hayo ndipo nilipoenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkuyuni-Sokoni ili wafanye utaratibu wa kukitoa hapo:”

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Mkuyuni, Godwin Peter Kyangara, amesema: “Mimi nimeletewa hizi taarifa za mtoto huyu aliyetupwa maeneo haya mida ya saa 2:30 asubuhi, baada ya kupokea taarifa hizo ikabidi nikatoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ndipo walipokuja kuuchukua mwili wa mtoto huyo.”

Inasemekana kwamba mtoto huyo alikuwa tayari ana umri wa miezi tisa hivyo mzazi wake alikuwa tayari amejifungua ndipo alipoamua kumtelekeza kwenye shimo hilo la kutupa takataka.

Kwa upande wake, diwani wa kata ya Mkuyuni, Charles Fashion, ameeleza kuwa ameshangazwa na kitendo hicho cha mwanamke kujifungua mtoto na kumtupa jalalani ambapo alisema inabidi atafutwe na apewe adhabu iwe fundisho kwa akina mama wengine wenye tabia kama hizo katika jamii.

Aidha, Jeshi la Polisi jijini Mwanza limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa bado juhudi za kumtafuta mwanamke huyo aliyetenda unyama huo zinaendelea ili afikishwe mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.


Wakazi wa Mkuyuni jijini Mwanza wakiwa katika eneo alilotupwa mtoto wakisubiri polisi.

Polisi akishirikiana na wananchi kuuchukua mwili wa mtoto huyo katika jalala alipotupwa na mama yake mzazi.

...wakisaidiana kuubeba mwili wa mtoto.

...wakielekea kwenye gari la jeshi la polisi.
...wakiupakiza mwili kwenye gari la jeshi la polisi.
...wananchi wakitaharuki kutokana na kitendo hicho cha mama kumtupa mwanaye dampo.

Mwili wa mtoto huyo ukiwa kwenye gari la polisi.


...gari la polisi likiondoka katika eneo la tukio.


...wananchi wakisambaa kutoka kwenye eneo la tukio.
Wananchi wakijadiliana baada ya tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment