
Richard Bukos na Issa Mnally Dada mmoja aliyedaiwa kuwa mjamzito usiku wa Ijumaa iliyopita alizua tafrani na kusababisha onesho la Yamoto Band kusimamishwa baada ya kuvamia jukwaa na kufanya ndivyo sivyo huku kitumbo chake kikiwa kimejichomoza kiuchokozi kufuatia kuachwa wazi. Kisa hicho cha kushangaza kilitokea ndani ya Ukumbi wa White House uliopo Kimara jijini Dar ambapo Yamoto Band kwa kushirikiana na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’...