Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, June 9, 2015

WATOTO WANUFAIKA NA DAWA MPYA ZA ARV

Dawa mpya za ARV kwa watoto ambazo azina ladha kama za zamani

Watoto walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa za kupunguza makali.
Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa Mradi wa Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono mpango wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''.
Na: Lonely Nzali                                                                               Chanzo: BBC SWAHILI                                                                           

0 comments:

Post a Comment