Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Saturday, June 6, 2015

MSAFARA WA MAKONGORO NYERERE WAPATA AJALI KASULU - KIGOMA


Gari lilivyopata ajali.

Wananchi wa Kasulu na Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio.

MSAFARA wa Makongoro Nyerere ambaye ni miongoni mwa wagombea urais, umepata ajali ya kupinduka kwa gari wilayani Kasulu mkoani Kigoma leo.

Ajali hiyo imetokea wakati Makongoro na msafara wake walipokuwa wakitoka mkoani Geita kuelekea Kigoma ikiwa ni katika harakati za kusaka wadhamini wake watakaomuwezesha kujaza fomu kuwania urais.

Taarifa zinasema kuwa, majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya matibabu.

Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema Jeshi la Polisi Mkoani humo litatoa taarifa kamili baadaye, baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

0 comments:

Post a Comment