Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, June 2, 2015

KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARADHI YA FISTULA YAENDELEA WILAYANI UVINZA-KIGOMA


Wakazi wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon (wapili kutoka kushoto ) alipokuwa akiwafafanulia jambo wakina baba hao kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha wakina baba na wananchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi fistula kwani yanatibika, Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.


Meneja Mawasiliano wa Hospitali ya CCBRT Abdul Kajumul , akiwaelezea wakazi wa kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Kigoma waliofika kwenye mkutano na kupatiwa elimu kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha wakina baba na wanchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi ya fistula bure katika hospitali ya CCBRT kwani yanatibika, Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.

Msanii wa nyimbo za kiasili na Balozi wa maradhi ya Fistula Mrisho Mpoto akitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Nguruka wilaya ya Uvinza Kigoma, Kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha wakina baba na wanchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi ya fistula bure katika hospitali ya CCBRT kwani yanatibika,Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.
Umati wa wakazi wa kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Kigoma wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi ya Fistula yanayowakabili wanawake hapa nchini,Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wakina baba kuwaruhusu wakina mama wajitokeze ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.

0 comments:

Post a Comment