Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, June 12, 2015

NISHA, SAJENTI WAWACHANA MASTAA KUCHAGUA MSIBA


Msanii wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.

Gabriel Ng’osha na Gladness Mallya
Wasanii wa Filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ na Husna Idd ‘Sajenti’ hivi karibuni wamewachana wasanii wenzao kuwa ni watu wa kuchagua misiba.

Wasanii hao waliongea hayo walipokuwa kwenye msiba wa msanii aliyewahi kutamba na Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Mzee Kankaa aliyefariki dunia siku ya Jumanne nyumbani kwake Tandale jijini Dar.


Husna Idd ‘Sajenti’.

Nisha alisema: “Wasanii tunapaswa kuwa na ushirikiano katika shida na raha, hasa kwenye misiba ya wenzetu, leo yeye kesho mimi, au wewe. Tuache kuchagua misiba siyo ubinadamu.’’

Sajenti naye alishadadia: “Haipendezi kuona wasanii tunapendana wakati wa uzima tu, mwenzetu anapofariki hatujitokezi kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho, tunaishia kuangalia aliyekufa ni nani ana mashabiki kiasi gani.”

0 comments:

Post a Comment