Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, June 2, 2015

VIFO VYA WATOTO WENGINE WAWILI VYATIKISA DAR!

Stori: Haruni Sanchawa
NImajonzi tena! Simanzi kubwa ilitawala kwa wakazi wa Jiji la Dar hususan Ukonga Mazizini kufuatia familia ya Emanuel Chadaha kufiwa na watoto wao wawili, Boniface (6) na Kelvin (4) katika tukio moja la kuzama kisimani.


Majeneza yaliyobeba miili ya watoto hao yakiandaliwa kwa ajili ya mazishi.

Vifo hivyo ambavyo vimeacha historia ya kusikitisha, vilitokea Mei 23, mwaka huu tena kwa mateso makubwa kwa vile wakati wanazama mmoja mmoja ndani ya kisima hicho hawakupata msaada wowote.Kwa mujibu wa waombolezaji kwenye msiba huo, watoto hao ambao walikuwa wakipendana sana, siku ya tukio walikuwa wakicheza nje ya nyumba yao huku baba yao mzazi, Emanuel akiwa ndani akizungumza na mgeni.

“Baba yao kwa vile aliona hali ya hewa nje si nzuri, mvuamvua ilikuwa ikinyesha, aliwaonya watoto wake wasichezee nje.
“Baba yao aliwazuia mara tatu lakini si unajua watoto tena, waliendelea kucheza nje.

“Nyumba wanayoishi, kwa pembeni kuna kisima ambacho hakijafunikwa juu na mbaya zaidi kilijaa maji, sasa kwa uelewa wa watoto hao waliamini kisima hicho hakijajaa,” alisema mwombolezaji mmoja.Simulizi hii ya watoto, iliendelea kusema kuwa, baba wa watoto haoa alianza kuhisi utulivu uliopo nje si wa kawaida hivyo kudhani kwamba watoto wake walikwenda kucheza mbali.


Waombolezaji wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kuaga miili ya watoto hao.

Alitoka nje kuwaangalia hakuwaona, akaenda kwa majirani ambako pia hawakuwepo. Alipokuwa akipita usawa wa kisima, alishtuka kuona kandambili moja ya Kelvin ikielea.“Kama mzazi mwenye uchungu tayari alishahisi mauti imemfika mtoto wake, akachukua uamuzi ya kuingia ndani ya kisima ambapo aliwakutana watoto wake wote wameishakunywa maji, alipoibuka akapiga kelele.

“Majirani tulijitokeza baada ya kuomba msaada, tukawatoa na kuwakimbiza Hospitali ya FFU Ukonga (Dar) lakini madaktari walisema walishafariki dunia hivyo miili ikapelekwa Hospitali ya Amana kwa ajili ya kuhifadhiwa.
“Inavyoonekana, aliyeanza kuzama ni mkubwa, mdogo wake alipoona kaka yake amezama na yeye akajitosa ili kumwokoa, kumbe naye anaitwa na mauti,” alisema jirani mmoja.

Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, watoto hao walikuwa wawili waliozaliwa tumbo moja, hivyo wazazi hao wamebaki watupu. Inauma sana!Mama mzazi wa watoto hao, Vailet Muhaha aliposikia watoto wake wamefariki dunia alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitali kiasi cha kumfanya ashindwe kuaga miili ya watoto hao.

Watoto hao waliagwa Mei 27, mwaka huu katika Kanisa la Angalikana, Ukonga na kusafirishwa kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi yaliyofanyika siku iliyofuata.
Mungu azilaze pema peponi, roho za watoto hao. Amina.

0 comments:

Post a Comment