Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, June 12, 2015

TANZIA: MENEJA WA JAMBO LEO, RAMADHANI KIBANIKE AFARIKI DUNIA



Marehemu Ramadhani Kibanike enzi za uhai wake.


Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky na Mwandishi wa Habari, Stela Kessy (kulia), wakiendelea na kazi huku wakiwa na huzuni baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Kibanike jana jioni.

Mwanahabari Celina Mathew akilia kwa uchungu baada ya kupokea taarifa hiyo.

Ofisa Matangazo, Kinai akiwa amepigwa butwaa kutokana na kifo hicho.


Wanahabari Nyendo Mohammed (katikati), Edith Msuya (kulia) na Magendela Hamisi wakiwa katika hali ya huzuni kufuatia kifo hicho.

Mwanahabari Magendela Hamisi akitafakari juu ya kifo hicho.

Msanifu kurasa wa gazeti la Jambo Leo, Elizabeth Mkeleja alishindwa kujizuia kulia.

Dereva wa Ramadhani Kibanike akiwa katika huzuni baada ya kupokea taarifa ya kifo hicho.

Mwanahabari Grace Gurisha akisaidiwa na wenzake baada ya kuishiwa nguvu muda mfupi baada ya kupata taarifa hizo za kifo cha Ramadhani Kibanike.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya JL Comunications inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, imepata pigo baada ya aliyekuwa Meneja wake Mkuu, Ramadhani Kibanike kufariki.
Kibanike alifariki dunia jana mchana nyumbani kwake Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akitoa taarifa ya kifo hicho kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Theophil Makunga alisema Kibanike alikumbwa na mauti jana mchana.

Mipango ya mazishi bado inapangwa, na msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Jijini Dar es Salaam.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

0 comments:

Post a Comment