Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Saturday, June 6, 2015

MAZISHI YA KAMISHNA MKUU MSTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA YAFANYIKA MOSHI


Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiweka jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa kwenye nyumba yake ya milele. Mazishi hayo yamefanyika jana Juni 05, 2015 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.


Askofu Mstaafu Dkt. Martin Shayo wa Dayosisi ya Kasikazini akiongoza Ibada Maalum ya mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye amefariki Juni 2, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi ka Magereza, John Casmir Minja.


Kabuli la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa limepambwa na mashada ya maua baada ya mazishi.

0 comments:

Post a Comment