Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, June 2, 2015

WAATHILIKA HAWA WA MADAWA YA KULEVYA MCHUNGAJI ATAJWA


Na Makongoro Oging’
Baadhi ya waathirika wa madawa ya kulevya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam ambao kwa sasa wameachana na matumizi ya madawa hayo walimtaja mchungaji wa kanisa moja (jina linahifadhiwa) ambaye alikamatwa na serikali na kwa sasa kesi yake inanguruma Mahakama Kuu jijini hapa.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Said Ismail Ngindo.
Waathirika hao ambao wako katika kikundi chao kijulikanacho kwa jina la Wanamati, walimueleza mwandishi wetu wiki iliyopita kuwa mchungaji huyo lazima abebe lawama zao kwa kuwa alikuwa akiwasambazia madawa hayo yaliyowafanya waathirike.
Waathirika ambao wapo zaidi ya 500 waliyasema hayo mara baada ya kumaliza kikao chao ambacho kilikuwa kikijadili jinsi ya kujikwamua baada ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.Waathirika hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini kwa sababu za kiusalama, walisema mchungaji huyo alikuwa akiwauzia madawa hayo mitaani kwa kuwatumia mawakala wake ndipo polisi waliamua kumfuatilia na kumkamata na kwa sasa ana kesi Mahakama Kuu.

Mmoja wa waathilika wa dawa hizo.
Hata hivyo, waathirika hao wameiomba serikali na taasisi mbalimbali kuwasaidia kimaendeleo kupitia kikundi chao hicho kwa kuwa wameachana na utumiaji wa ‘unga’ na wangependa wajitegemee kwa kufanya shughuli za kuzalishaji mali.
Waathirika hao ambao wengi wao wamesema kwa nyakati tofauti kuwa wamekuwa wakitumia unga kati ya miaka mitano hadi ishirini na kwamba jamii isiwachukie kwa maana na wao walirubuniwa bila kujua madhara ambayo wangeweza kuyapata lakini kwa sasa wako vizuri kwani wamekuwa wakihudhuria kliniki katika Hospitali ya Temeke, Dar.
Wameiomba serikali iendelee kuwapatia dawa za kutibu utumiaji wa madawa kwa kipindi chote cha miaka miwili wanayotakiwa kutumia ili waweze kurejea katika hali yao ya zamani.Mwenyekiti wa kikundi hicho, Said Ismail Ngindo alisema kwamba wameamua kuungana kwa pamoja ili waweze kufanya shughuli za maendeleo baada ya kuachana na madawa na wameiomba serikali iwasaide ili wajikwamue kiuchumi.

Wakiwa kwenye kikundi chao.
“Asilimia kubwa ya wanachama wa kikundi hiki hawana ajira…ni kazi ngumu sana kukaa bila kuwa na kipato, hapa kuna akina mama ambao wamezalishwa kipindi hicho wakiwa watumiaji wa madawa mitaani, sasa wanapata shida kubwa ya kuwalea watoto wao, hivyo kunahitajika msaada mkubwa, “ alisema mwenyekiti huyo.
Taarifa iliyopatikana ndani ya kikundi hicho inasema kwamba imefikia hatua ya viongozi wa kikundi  walioteuliwa na uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke kuwasimamia  wenzao lakini wao wamewachagua viongozi wao ili wawe wakiheshimika zaidi na wana kikundi.

0 comments:

Post a Comment