Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, June 2, 2015

MELI ILIYOKUWA NA WATU ZAIDI YA 450 YAZAMA NCHINI CHINA


China
Meli ya Dongfangzhixing ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imepinduka na kuzama jana usiku baada ya kukumbwa na dhoruba la upepo mkali katika mto Yangtze kusini mwa China.

Taarifa zimeeleza kuwa, meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Mashariki mwa Mji wa Nanjing kwenda Chongqing Kusini Magharibi mwa China ndipo ilipozama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.

Meli hiyo ya Dongfangzhixing au Nyota ya Mashariki ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa Shirika la Usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Serikali ya China, Xinhua ni kwamba, kifaa maalum cha kurekodia video (CCTV Camera) kimeonesha watu watano wakiwa mamefariki dunia kutokana na ajali hiyo na18 wakiwa wameokolewa mpaka sasa. Kikosi cha Uokoaji kinaendelea na juhudi za uokoaji kwa abiria wengine ambao hawajapatikana mpaka sasa. Japo kazi ya uokoaji inakwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa zinazonyesha.

Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang amedfika eneo la tukio na kujionea maafa hayo.

Kwa upande wao Nahodha na Mhandisi Mkuu, ambao ni miongoni mwa waliookolewa wamekaririwa wakisema kuwa, meli ilikumbwa na kimbunga kikali ikapinduka na kuzama wakati huohuo.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.

Inasemekana kuwa, waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya Shanghai.

Ikumbukwe kuwa, mwezi Januari watu 22 walifariki dunia kwenye mto huo wakati boti iliyokuwa kwenye majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang, katika jimbo la Jiangsu.

NA BBC

Mwanamke aliyekuwa amezama akiokolewa.


Kikosi cha waokoaji katika mto Yangtze wakiendelea na shughuli ya uokoaji.


Kikosi cha uokoaji kikijiandaa kwenya kuwatafuta waliozama kwa ajali hiyo.


Meli ya Dongfangzhixing iliyozama.

Shughuli za uokoaji zikifanyika.


Kikosi cha Uokoaji kikiwa kazini.


Juhudi za uokoaji zikiendelea.
Boti maalum za uokoaji.


Waandishi wa habari wakichukua tukio hilo.


Meli iliyozama.
Mmoja wa wahanga wa ajali hiyo akifungwa kamba ili aokolewe kutoka majini.

...akiokolewa.
Kikosi cha uokoaji cha dharula wakiendelea na oparesheni katika mto Yangtze.


Wanakiji wawili wa China wakitazama tukio hilo.

Majeruhi katika ajali hiyo akipelekwa kwenye huduma.


Ndugu wa baadhi ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo wakiwa na simanzi.
Simanzi na majonzi.

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang (aliyeketi) akiwa kwenye Mkutano huko Beijing wakipanga mkakati na namna ambavyo uokoaji utafanyika.

0 comments:

Post a Comment