Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, June 12, 2015

JINSI YA KUKABILIANA NA TATIZO LA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI

Hili ni tatizo linalosababisha ugumba kwa wanawake kwa kiasi kikubwa. Wanawake wanaoshindwa kupata ujauzito hukabiliwa na matatizo matatu; Kwanza kabisa ni kuziba kwa mirija ya mayai kama tutakavyoona leo na pili ni matatizo katika mfumo wa homoni ambapo kuna sababu zake tutakuja kuziona katika matoleo yajayo.

Hata hivyo, dalili kuu ni kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopata hedhi na kupata damu kwa muda mrefu au muda mfupi sana ambazo ni siku moja au mbili.

Dalili nyingine ambazo siyo nzuri katika mfumo wa homoni ambazo zinaweza kufanya mwanamke asipate mimba ni matiti kutoa maziwa wakati siyo mjamzito na wala hana mtoto anayenyonya.

Tatizo lingine la tatu ni kwa upande wa mwanaume kutokuwa na mbegu zenye ubora.
Yaani hana nguvu za kutosha au anawahi kumaliza tendo la ndoa ‘premature ejaculation’ kama tulivyoona hapo awali.
Kuziba mirija ya uzazi huzuia mbegu na mayai kukutana na kutungisha mimba. Mirija ya uzazi pia huitwa Oviducts, Uterine tubes au Salpinges.

AINA ZA UZIBAJI WA MIRIJA
Tumeona sababu kuu tatu zinazomfanya mwanamke asipate mimba. Kuziba kwa mirija ya uzazi huchukua asilimia ishirini ya tatizo la ugumba kwa mwanamke au mwanamke kupoteza uwezo wa kuzaa, pamoja na hizo sababu tatu, pia zipo sababu nyingine ndogo nyingi ambazo tutakuja kuziona kwa undani katika uchambuzi ujao.

Aina za uzibaji ni mirija kuziba upande wa mwishoni karibu na vifuko vya mayai ‘Distal tubal occlusions.’
Hali hii inahusiana kabisa na tatizo la mirija kuvimba au kujaa maji hali iitwayo kitaalamu Hydrosalpinx ambapo pamoja na mwanamke kushindwa kupata mimba, pia husumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara yanayosambaa kulia na kushoto.

Hali ya kuvimba kwa mirija au mirija ya uzazi kujaa maji husababishwa na maambukizi ya vimelea vya ‘Chlamydia trachomatics’.

Katika hali hii pia huweza kutokea hali ya kizazi na viungo jirani kushikamana hivyo mirija pia hushikwa na kuziba.
Hali hii ya kuziba mirija mwishoni husababisha sehemu ya mirija iliyo kama vidole iitwayo ‘fimbriae’ kugandamana na kusababisha kushindwa kuchukua yai lililopevuka na kuliingiza katika mirija tayari kwa kutungisha mimba. Tatizo hili linapotokea, sehemu nyingine ya mirija inakuwa wazi au nzima. Mrija unaweza kuziba katikati ‘midsegment’ ambapo sababu kubwa inaweza kuwa mrija kufungwa au kukatwa kama njia ya kufunga uzazi. Mrija unaweza kuziba mwanzoni na sababu kubwa ni maambukizi kwenye kizazi kutokana na utoaji au kuharibika mimba na maambukizi mengine sugu ya kizazi.

0 comments:

Post a Comment