Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, June 12, 2015

WAGOMBEA URAIS WAMIMINIKA KWA MTABIRI

Gladness Mallya na Mayasa Mariwata

MAJANGA! Wakati vuguvugu la kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais likiendelea, imegundulika kuwa wagombea wengi wa urais wamekuwa wakimiminika kwa mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahaya, (pichani) maeneo ya Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutabiriwa safari yao hiyo, Ijumaa lina mkanda kamili.

Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hussein Yahaya.

Gazeti hili lilifanya uchunguzi wa kina baada ya kupata habari kutoka kwa watu wanaoishi jirani na mtabiri huyo kwamba wagombea kibao wanamiminika kwake ambapo lilifanikiwa kuwaona baadhi (majina tunayaifadhi) wakiingia katika ofisi ya mtabiri huyo kutabiriwa mambo yao kuelekea kwenye kugombea nafasi ya urais.

Mgombea mmoja alifika kwa mtabiri huyo akiwa katika gari la lenye vioo vyeusi (namba zake zinahifadhiwa) na aliongozana na mpambe mmoja.Mgombea urais mwingine aliyekuwa na nywele ndogo alifika katika ofisi za mtabiri huyo akiwa na mwanamke, haikuweza kufahamika kama ni mkewe au la.


Lowassa

“Hao mliowaona ni wachache mbona hapa wanapishana usiku na mchana na wengine wengi wanaogopa kuja mchana wanamuomba mtabiri abaki mpaka usiku mwingi ndiyo wanakuja, yaani hawa wagombea urais wanahangaika kweli,” alisema jirani mmoja kwa sharti la kutotajwa jina.

Baada ya uchunguzi huo, mapaparazi wetu walifika ofisini kwa mtabiri huyo na kumuuliza kuhusu wagombea wanaofika kwake kwa ajili ya kutabiriwa mambo yao kuhusu urais ambapo maalim Hassan alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli wanakuja wengi sana lakini siwezi kukutajia majina yao maana ni kinyume cha maadili ya kazi yangu.
“Kwenye astrology (unajimu), kuna mengi na ndiyo maana wanakuja kwangu.


Membe.

Nikufahamisheni tu kwamba enzi hizo baba yangu Sheikh Yahya Hussein alikuwa anawatabiria marais kama vile Jomo Kenyatta (Kenya), Wiliam Tolbert (Liberia), Mfalme Sebhuza (Swaziland) na kadhalika, kwa hiyo siyo ajabu hawa kuja kwangu,” alisema Maalim Hassan.
Picha zilizotumika mbele za wagombea siyo waliokwenda kwa mtabiri.

0 comments:

Post a Comment