Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Thursday, January 1, 2015

TAMBUA VIMBE MBALIMBALI KWA MWANAMKE NA JINSI YA KUZIONDOA PASIPO UPASUAJI-3


Baada ya wiki iliyopita kuelezea dalili za vimbe katika mwili wa mwanamke, leo hii tunaendelea vipengele vingine.

Fibroids au Mayoma
Hizi ni vimbe zinazotokea katika mji wa mimba na hizi ndizo vimbe zinazowasumbua watu wengi sana katika jamii yetu ya sasa, na dalili zake ni kama;

Mwanamke hupatwa na maumivu chini ya kitovu lakini ni katikati siyo upande wa kulia wala upande wa kushoto na mara nyingi maumivu haya huambatana na maumivu ya kiuno, maumivu ya mgongo na maumivu hayo huenda hadi sehemu za mapaja na kushuka hadi miguuni na maumivu haya huwa makali sana hasa wakati wa hedhi. Ukiona unaandamwa na dalili hizi basi ujue kuna uwezekano ukawa na Fibroids au Mayoma.

Kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo, mwanamke ukiona tumbo linaongezeka ukubwa na unasikia kama kuna kitu kinatembea ndani ya tumbo, wakati huohuo unaandamwa na maumivu makali chini ya kitovu kwa katikati na maumivu makali sana wakati wa hedhi basi ni dalili kubwa nawe ukawa na Fibroids au Mayoma.

Polycystic ovarian syndromes {PCOS} au Multiple cysts
Hizi ni zile vimbe ndogondogo nyingi zinazoweza kutokea kwenye kifuko cha mayai cha mwanamke, lakini nazo pia huweza kutokea katika pande zote mbili za vifuko vya mayai kwa mwanamke. Nazo zina dalili zake mbalimbali, nazo ni kama;

Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi katika mwili wake hasa kwenye mikono au kwenye miguu au anakuwa na ndevu au kifuani (garden love) na hii ni kwa sababu mwanamke huyu anakuwa na hormone nyingi sana za androgen yaani anakuwa na hormone nyingi za kiume, basi ukiona dalili kama hizo ni vema kuwahi hospitali.

Pia kuna hali ya kuvurugika hedhi ya mwanamke na kuwa haieleweki na pia kuwa na maumivu ya kiuno upande wa kulia au wa kushoto nayo pia inakuwa ni dalili kubwa sana ya PCOS au Multiple cysts hivyo ni vema kuchukua hatua za haraka.

Hali ya kutokwa na uchafu sehemu za siri kwa mwanamke ni moja ya dalili hasa uchafu huo unapokuwa hauna harufu na wala hauwashi basi ujue kuwa kuna uwezekano mkubwa nawe ukawa na PCOS au Multiple cysts.

Hydrosulpinx.
Hii ni ile hali ya mwanamke kujaa maji katika mirija yake ya kizazi na mirija hiyo inakuwa haipitishi mayai ya uzazi. Dalili yake kubwa ni kuwa na maumivu makali sana kwenye kiuno ambayo huweza kutokea upande mmoja au yakatokea pande zote mbili na huenda hata maumivu yanayotokea upande, yote haya yanaisha bila kufanya upasuaji.

Dalili zipo nyingi sana na tukianza kuziongelea zote basi inaweza kuchukua mwezi. Lakini tutaishia hapa na wiki ijayo tutaendelea na VYANZO VYA VIMBE KATIKA MWILI WA MWANAMKE.

0 comments:

Post a Comment