Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, January 9, 2015

KIJANA ANG'ATWA KIDOLE KISA CHIPSI


Abdul akionyesha kidole kilichokatwa katika tukio hilo.

STORI:ISSA MNALLY
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Abdul mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akiukaribisha vibaya mwaka wa 2015 baada ya kung’atwa kidole kimoja cha mkono wa kulia mpaka kukatwa.

Tukio hilo la kustaajabisha lilitokea maeneo ya Corner Baa iliyopo Sinza Africa-Sana majira ya saa saba usiku wa kuamkia Jumatatu, Januari 5 ambapo aliyemfanyia kitendo hicho ni kijana ambaye jina lake halikupatikana mara moja.


Akionyesha kidole kilichojeruhiwa.

Chanzo kilichokuwa eneo la tukio kilieleza kuwa, awali mtuhumiwa alifika maeneo hayo kwa lengo la kutaka auziwe chipsi lakini kitendo cha kucheleweshewa huduma kilimkera.

“Unajua jamaa inaonekana alikuja kwa shari, yaani alipocheleweshewa chipsi zake, akaanza kuwaka.
“Hata alipopewa alilalamika kupunjwa, basi ikasababisha hali ya kuzinguana kati ya yule mnunuzi na muuzaji. Hee.. si tukashangaa yule jamaa akamng’ata muuza chipsi kidole kisha akatema kipande,” akaeleza mtoa habari huyo.


Kijana aliyemng'ata mwenzie kidole akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Ikaelezwa kuwa, baada ya kuona damu zimetapakaa mahali hapo, wasamaria wema walimpeleka Abdul katika dispensari ya karibu na kwa bahati nzuri askari waliokuwa doria walipita na kukuta tukio hilo hivyo kumchukua mtuhumiwa na kwenda naye Kituo cha Polisi Mabatini.

0 comments:

Post a Comment