Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, January 13, 2015

SEIF SUDI SEIF (15) NATESEKA JAMANI NA MGONGO, NISAIDIENI

INASIKITISHA! Mtoto Seif Sudi Seif, 15, (pichani), wa Shule ya Msingi Hedenzeri, Tanga analia kwa uchungu akitaka kusaidiwa ili aweze kutimiza ndoto zake kutokana na tatizo lake la kushindwa kutembea kutokana na kuumwa mgongo.

Mtoto Seif Sudi Seif akishindwa kutembea kutokana na tatizo la mgongo.


Mama wa mtoto huyo, Fatuma Hemed aliliambia gazeti hili akiwa nyumbani kwa shemeji yake maeneo ya Uwanja wa Ndege jijini Dar, alikofikia akitokea Tanga, kuwa tatizo la mwanaye lilianza miaka minne iliyopita na sasa anashindwa kutembea.

Akifafanua zaidi alikuwa na haya ya kusema: “Kabla ya mwanangu hajakumbwa na tatizo hili alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuanguka akidai kuona kizunguzungu hadi kushindwa kabisa kutembea na sasa hushinda amelala, anashindwa hata kuinuka.

“Ni tatizo zito na kwa upande wa masomo anajitahidi sana katika mitihani yake shuleni japokuwa anapata shida kubwa ya kukokota baiskeli ya kusukuma kutokana na mgongo wake kutokuwa imara kusimama,” alisema mama huyo.

Mtoto Seif Sudi akiwa na mama yake.


Naye mtoto Seif alisema kuwa anatamani sana kurudia katika hali yake ya zamani na angependa kutimiza ndoto zake za kusoma hadi chuo kikuu.“Lakini ndoto hizo nitashindwa kutimiza kutokana na kuumwa na sasa nashinda kitandani nimelala bila kuinuka wala kutembea.

“Mama amenipeleka hospitali mbalimbali kama vile Mkoa wa Tanga, Hospitali ya Mombo pamoja na Dar, Hospitali ya CCBRT, Tumbi ya Kibaha lakini imeshindikana kwa kuwa hata hivyo, uwezo hana.
‘’Nawaombeni Watanzania mnisaidie niweze kutimiza ndoto zangu kwani nimehangaika sana, mama yangu amehangaika,’’ alisema Seif.

Mama wa mtoto huyo alisema ameambiwa na madaktari kuwa tatizo la mwanaye ni ‘mgongo kusogea’ na anaweza kutibiwa nchini India.Yeyote atakayeguswa na tatizo hilo awasiliane na mama wa mtoto kwa namba 0653 542 128 au 0715 125 703 Fatuma Hemed.

0 comments:

Post a Comment