Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, January 26, 2015

MIMBA KUYEYUKA (BLIGHTED OVUM) INATOKEAJE?


TATIZO hili pia huitwa ‘anembryonic gestation’. Hutokea pale mfuko wa mimba unapoendelea kukua bila ya kuwa na mtoto ndani. Kifuko cha mimba huitwa ‘gestational sac’ na mtoto ni ‘embryo’.

HALI HALISI
Mwanamke anakuwa mjamzito ambapo ana dalili zote za ujauzito na katika wiki sita za mwanzo akifanya Ultrasound mtoto anaweza kuonekana lakini baada ya hapo dalili za mimba zinaanza kupungua taratibu na mama akifanya Ultrasound mimba itaonekana mfuko wake tu lakini ndani hakuna kitu!

MWENDELEZO
Hapa ndipo tunasema mama amepata blighted ovum. Mimba ilikuwepo lakini imeyeyuka! Hali hii ikiendelea mama ataanza kutokwa na damu taratibu.Wakati mwingine anaweza kupatwa na tatizo hili hata bila yeye mwenyewe kujijua kama ni mjamzito.

HUKATISHA TAMAA
Blighted ovum ni tatizo linalokatisha tamaa kwa mwanamke anayetafuta ujauzito na wakati mwingine haamini kilichotokea.

NINI SABABU?
Tatizo hili hutokana na hitilafu katika yai lenyewe kutokana na kasoro za kromozom zinazorutubisha yai. Kromozom zinazorutubisha yai ni za kiume zikiungana na za kike, hivyo mimba ikitungwa na kasoro haiendelei, inatoka mapema. Mwanamke anaweza kutokewa na tatizo hili hata zaidi ya mara mbili.
Kasoro za kromozon zinaweza kusababishwa na mambo mengi kama maambukizi, kemikali na mionzi au hali isiyoeleweka.Kromozom za kiume na za kike pia huchangia hali hii. Kromozom za kike ni aina ya X na zile za kiume ni za aina ya Y.

HALI YA MWANAMKE
Mwanamke ana aina moja tu ya kromozom ambazo ni za kike na mwanaume ana kromozom za aina mbili, za kiume na kike. Kromozom pia zikichoka husababisha mimba iwe na kasoro hivyo huharibika na kutoka.
Kama tulivyoona, mimba inaweza kuyeyuka ghafla na mwanamke anaweza kupoteza hata mimba tatu au zaidi.

Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment