Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, January 7, 2015

JINSI YA KUPUNGUZA UNENE WA KUPINDUKIA


UNENE wa kupindukia ni ugonjwa na wasomaji wengi wametaka tuwasaidie kuwaeleza njia za kupunguza au kuondoa tatizo hilo.Kuna njia nyingi sana ambazo hutumiwa na watu ili kupunguza mwili na tumbo, lakini baadhi huwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanayoishi, hivyo wengi hushindwa njiani.

Zipo njia za kutumia madawa au kahawa, chai ya kupunguza uzito na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu na hata baadhi huwa na madhara.Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyohivyo bila kuongezeka uzito wa mwili.

Tutatoa mfano wa kupunguza uzito kwa muda wa siku 7. Mambo muhimu ya kuzingatia ni kwamba, kupungua uzito kunategemea kiwango cha mafuta mwilini (body fat), uzito wa mtu, kalori anazohitaji kwa siku, BMI yake pamoja na lengo la mtu kutaka kupunguza uzito.

Nahitaji kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa kiasi gani? Kwa mfano wengine wanahitaji kupunguza asilimia 10, 20 au 25 ya kiwango cha mafuta mwilini. Kwa maana hiyo, si kila mpangilio wa ulaji (diet plan) humfaa kila mtu, inaweza ikawafaa baadhi na isiwafae wengine.

Jambo lingine la kuzingatia ili kupungua uzito ni kufuata ushauri wa wataalamu wa lishe, madaktari, wataalamu wa mazoezi na kadhalika. Ufuatao ni mfano wa njia ya kupunguza unene au diet plan. Kila siku unahitaji kunywa kikombe kimoja cha kahawa na ni vizuri kubadilisha unywaji wa kahawa kwa chai, yaani kama leo utakunywa kahawa kesho kunywa chai na kadhalika.

Kwa wale wenye ugonjwa wa shinikizo la damu, ugonjwa wa wasiwasi na kadhalika, wanashauriwa kuepuka kahawa kabisa na hivyo wanywe chai. Wagonjwa wa kisukari wanaweza kunywa chai au kahawa kwa kukamulia ndimu au limao ndani yake na hivyo kuongeza ladha.
Siku ya kwanza:

Mazoezi: Wale wenye matatizo ya kiafya ya mapigo ya moyo au wale ambao walishawahi kuugua hapo awali matatizo ya moyo na wagonjwa wa pumu, ni vyema wafanye mazoezi chini ya uangalizi wa wataalamu wa mazoezi pamoja na kushauriana na daktari.

Tembea kwa muda wa dakika 30 asubuhi au jioni kabla ya kula chakula chochote. Kwa wale wenye mashine ya kutembelea ya tredmill wanaweza kutembea kwa muda wa dakika 30 kwa kuanza na kasi ndogo. Unaweza pia kukimbia kwa muda wa nusu saa au kukimbia kwenye mashine ya tredmill kwa muda wa nusu saa.

Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment